Afya

Jinsi ya Kupunguza Kitambi

Jinsi ya Kupunguza Kitambi

Jinsi ya Kupunguza Kitambi -Kupunguza kitambi/tumbo ni changamoto kubwa ni kitu ambacho kina tunyima amani wengi lakini namna ya kukipunguza huwa ni ngumu sana, wengi huwa tuna fanya diet au kuamua kwenda gym kweli zina weza kusaidia lakini kama huwezi hivyo vyote ni nini ufanye?

Jinsi ya Kupunguza Kitambi
Jinsi ya Kupunguza Kitambi

1. KUNYWA MAJI MENGI

Kunywa maji mengi mara kwa mara kwa siku itakusaidia kuto kusikia njaa

Hii itakufanya uwe mbali na vyakula vyakula vya hapa na pale visivyo kuwa na msingi lakini pia maji yana saidia kufanya ngozi iwe nyororo

2. PUNGUZA AU ACHA KUNYWA SODA

Sukari ni moja ya vitu vibaya vinavyo anzisha/kuleta unene kaa mbali nazo na anza kunywa maji kwa wingi

3. WEKA RATIBA YA CHAKULA

Ni vizuri kama utakuwa unajipikia mwenyewe maana utajua uweke chumvi, sukari kiasi gani, mafuta nk.

Pangilia ratiba yako ya week nzima lakini pia katika ratiba yako weka healthy food ambazo zitakufanya uweze kupuguza mafuta mwilini

4. ACHA KULA VITU VIDOGO VIDOGO

Biscuits, Big G, Chocolate ni vitamu na vina temptation sana lakini navyo vinaongeza sukari na kusababisha kuleta unene tumboni jaribu kuviepuka sana

5. JITAIDI ULE TARATIBU

Hapa huwa tunashindwa sana, lakini kula taratibu kuna saidia kumeng’enya chakula chako vizuri lakini pia kunafanya ule chakula kidogo na kushiba haraka.

6. EPUKA VYAKULA VYA MAFUTA

mafuta ni mabya sana katika chakula jaribu kutumia mafuta yenye less cholesterol, kama mafuta ya nazi, olive oil, almond au pika chukuchuku ukiongezea chakula chako na parachichi.

Parachichi linaweza kusababisha chakula kiwe kitamu na lina mafuta ambayo hayana madhara.