Afya

Dawa ya macho mekundu Red eyes

Dawa ya macho mekundu Red eyes -Ugonjwa wa Macho Red eyes Ugonjwa wa Macho Dar es salaam Dar -Macho mekundu” ni neno linalotumika kuelezea macho yaliyopata wekundu, kuwasha, na kuwa na viashiria vya damu (bloodshot).

Wekundu huu hutokea pindi vimishipa midogo ya damu chini ya uso wa jicho vinapotanuka au kuvimba. Mara nyingi, ni athari ya ukereketaji (irritation) au mashambulizi (infection) ya kwenye jicho. 

Kumbuka kuwa, kuna aina nyingi sana za macho mekundu, baadhi yake unaweza kujitibia wewe mwenyewe nyumbani na nyingine utajitaji msaada wa haraka wa daktari.

  • Pata mapumziko ya kutosha.
  • Weka kitambaa kizito juu ya macho yaliyofungwa.
  • Fanyia massage ngozi ya juu ya jicho (eyelid)
  • Kwa utaratibu kabisa safisha ngozi ya jicho (eyelid) kwa kutumia maji safi.
  • Unaweza kuweka matone ya dawa za kawaida (OTC).