Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi -Ikitokea mwanamke amepata ujauzito ambao hakutarajia, hasa kwenye mazingira ambayo hakuwa amejiandaa yeye binafsi hujilaumu sana.
Huu ndiyo wakati unaozaa kauli maarufu sana mtaani, “nimepata ujauzito kwa bahati mbaya”.
Hii ni kauli dhaifu, haina mashiko kisayansi.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Ujauzito siyo jambo la dharura wala bahati mbaya. Hutokea kwenye siku maalumu na mazingira sahihi.
Baadhi ya wanawake hupitia changamoto kubwa sana katika kupata ujauzito.
Wengine hadi sasa wanahangaika kuutafuta. Sina hakika kama ni wewe, lakini nafahamu kuwa andiko hili litakufaa pia.
Fanya mambo haya ili uweze kupata ujauzito kirahisi, pasipo kutumia nguvu kubwa sana. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
1. Siku za hatari
Hii ni kauli isiyo na usikivu mzuri kwenye masikio ya wasomi, kwa maoni yangu binafsi ingepaswa ziitwe siku za neema.
Ni siku zenye uwezekano mkubwa zaidi wa kupata ujauzito. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Kuna aina nyingi za mizunguko ya hedhi, baadhi ikianzia siku 21-35, na kila mzunguko huwa na siku zake za hatari.
Kushiriki tendo la ndoa kwenye siku za hatari kulingana na mzunguko wako huleta ujauzito wa haraka kuliko kufanya tendo la ndoa kila siku.
Jambo la kusikitisha ni kuwa wanawake wengi hawajui mizunguko yao, na wengine hudhani kuwa wanajua kumbe hawajui. ( 1, 2 )
Jifunze leo mzunguko wako, kisha tumia siku sahihi kikamilifu.
2. Mbegu za kiume
Mwanamke huwa hajiwekei ujauzito mwenyewe, ni lazima akutane kimwili na mwanamme ndipo ujauzito utungwe.
Hii inatoa maana kuwa mbegu za kiume ni lazima pia zitazamwe kwa jicho la pili.
Ni lazima mwanamme awe na mbegu bora, zenye maumbo sahihi, zinazozalishwa kwa namba inayotakiwa.
Ili kufanikisha haya yote, inapaswa mwanamme aishi mtindo bora wa maisha. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Uvutaji wa sigara na madawa ya kulevya, unywaji wa pombe nyingi, uzito mkubwa, lishe duni na uwepo wa baadhi ya maradhi hasa kisukari huathiri na kupunguza uwezo wa mwanamme katika kurutubisha yai la mwanamke. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Mwanamme anapaswa pia kutumia virutubisho na vyakula vinavyo boresha afya ya mbegu za kiume.
Vyakula jamii ya karanga, mboga za majani, matunda, asali pamoja na virutubisho vya foliki asidi, omega 3, zinc na vitamini C na E huongeza ubora wa mbegu za kiume. ( 3, 4, 5, 6, 7 )
3. Penda uke wako
Wanawake wengi hudhani kupenda sehemu zao za siri ni kujiwekea manukato yanayotoa harufu nzuri, kutumia kemikali kali kujisafisha pamoja na kuingiza vitu mbalimbali pasipo hata kujiridhisha na usalama wake.
Mazingira ya uke yameumbwa kiasili kuruhusu uogeleaji bora wa mbegu za kiume baada ya kumwagwa.
Kemikali nyingi wanazotumia wanawake kuingiza ukeni huharibu mazingira ya humo, husababisha magonjwa mbalimbali ya uke na baadhi huwa na sifa ya kuua mbegu za kiume hivyo kuchochea ugumba.
Unaweza kushangaa kwanini wewe ni msafi sana, mwanamme yupo vizuri pia na mnashiriki tendo la ndoa wakati wa siku za hatari lakini mimba haiji?
Kumbuka madude unayoingiza huko chini. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
Kutunza usafi wa sehemu hizi huleta siha njema kwa mwanamke, lakini uke umeumbwa kwa namna ya kipekee sana, unaweza kujisafisha wenyewe na mwanamke huhitajika kuusaidia kidogo tu kwa maji safi na sabuni isiyo na kemikali kali. ( 8, 9, 10 )
Punguza mbwembwe kwenye kujisafisha, unaharibu mazingira ya uke wako. Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
4. Stress
Umewahi kuwaza kwa nini wanawake wengi wanaolaumiwa na familia zao, au familia ya mwanamme kuwa kwanini hawapati ujauzito ndiyo hupitia changamoto kubwa zaidi ya kutatua tatizo hili kuliko wale wasio sumbuliwa na kulaumiwa?
Waza pia, kwanini mwanamke ambaye hana hata habari na ujauzito ndiye hunasa kirahisi kuliko yule anaye utafuta kwa nguvu?
Jibu ni stress.
Mwanamke anapokuwa na stress mwili huzalisha kiasi kikubwa cha vichocheo vya cortisol na epinephrine ambayo hupunguza usambazwaji wa damu, virutubisho, hewa na vichocheo vya mwili kwenda kwenye mfumo wa uzazi.
Aidha, stress husababisha pia kutokea kwa mvurugiko wa vichocheo vya mwili ambavyo kwa pamoja huathiri ubora wa afya ya uzazi wa mwanamke. ( 11, 12, 13 )
Najua unahangaika kutafuta ujauzito, pia una stress nyingi.
Nakuhakikishia kuwa ujauzito utaupata, ila tu ukikubali kupunguza stress.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
5. Kapime vichocheo
Mwili wa binadamu huongozwa na mifumo miwili ya taarifa ambayo ni mfumo wa neva za fahamu pamoja na mfumo wa vichocheo vya mwili, maarufu zaidi kama homoni.
Kwenye mambo ya uzazi, vichocheo au homoni za uzazi ndiyo huchukua nafasi kubwa katika kuamua uwezo wa mwanamke katika kubeba ujauzito.
Kama unapanga kupata ujauzito siku za hivi karibuni basi kapime homoni zako uone kama zipo sawa, kisha tulia.
Kama umehangaika kupata ujauzito lakini haujafanikiwa, uwezekano wa kuwa homoni za mwili wako hazipo sawa upo mkubwa. ( 14 )
Kapime pia, kisha tumia dawa utakazopewa.
Ukipona utakuwa tayari na nafasi kubwa ya kupata ujauzito.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
6. Uzito
Unafahamu kuwa wanawake wenye uzito mkubwa huwa na nafasi mara 3 zaidi ya kupatwa na tatizo la ugumba kuliko wanawake wenye uzito wa kiasi?
Wanawake wenye uzito mkubwa sana huhusishwa na tabia mbili zisizo na viashiria vizuri kwa afya yao.
Kwanza, wengi huwa na mizunguko ya hedhi isiyo imara, pili huwa na nafasi kubwa ya kupata siku za hatari ambao hutoa mayai yasiyo komaa.
Aidha, uzito mkubwa huchangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa tatizo la mvurugiko wa vichocheo ambalo tayari tumeshasema kuwa ni kikwazo kwa afya ya uzazi. ( 15, 16, 17, 18 )
Pambana sasa kuweka sawa uzito wako, itakusaidia kupata ujauzito haraka.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
7. Chunguza mirija
Kwenye mirija ya uzazi ndiyo sehemu ambayo ujauzito hutungwa, hii pia ni sehemu ambayo husafirisha mayai kutoka kwenye vifuko vyake kwenda kwenye mji wa uzazi.
Mirija hii hupaswa kuwa imefunguka kila mara, pia haipaswi kuwa na makovu, imeziba au imeshambuliwa na maambukizi ya aina mbalimbali za magonjwa.
Mirija iliyo wazi hurahisisha upatikanaji wa ujauzito, na kinyume chake ni sahihi pia. Chunguza mirija yako sasa, ikiwa imeziba fanya mpango izibuliwe. ( 19, 20, 21 )
Ikiwa imeshambuliwa na vimelea vya magonjwa tumia dawa sahihi utakazopatiwa ili kutibu changamoto hii.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
8. Tumia OPK’s
OPK’s ni ufupisho wa maneno Ovulation Predictor Kits, yaani vifaa maalumu vya kukuambia ni lini mwili wako una asilimia kubwa ya kupata ujauzito kwenye mzunguko wako wa hedhi kila mwezi.
Tulianza kwa kushauri kila mwanamke ajue mzunguko wa hedhi yake, na natumaini baada ya hapa juhudi zitafanyika katika kujifunza. ( 22 )
Kwa wale ambao zoezi hili litakuwa gumu kwao, au pia kwa baadhi ya wanawake wanaotaka kuwa na uhakika zaidi wanaweza kutumia hizi OPK’s.
Zipo za aina mbalimbali mtaani, ukienda pharmacy yoyote kubwa utazikuta.
Hizi zitakurahisishia kupata ujauzito kwa kuwa zitakupa taarifa sahihi za lini ushiriki tendo la ndoa ili ufanikiwe.
9. Virutubisho
Aina ya vyakula anavyotumia mwanamke, pamoja na virutubisho kwa ujumla wake huwa na mchango wa moja kwa moja katika kuboresha au kudumaza uhai wa afya ya uzazi.
Tafiti nyingi zinathibitisha kuwa ulaji wa nafaka nzima, mboga za majani , foliki asidi, omega 3, samaki, vitamini E na matunda huongeza ubora wa afya ya uzazi.
Kutokana na kukua uwanda wa tiba na sayansi shirikishi, baadhi ya makampuni yameweza pia kuzalisha virutubisho vinavyoweza kufanya kazi hii. Vitafute.
Mwanamke anashauriwa kutumia aina hii ya vyakula na virutubisho kabla hata hajaamua kupata ujauzito, lakini kwa wale wanaoweka mkazo baada ya kupitia changamoto za uzazi hawaja chelewa pia. ( 23, 24, 25 )
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
10. Uzazi wa mapango
Kuna baadhi ya njia za uzazi wa mpango ambao huwa salama kwa asilimia 100.
Mfano wa njia hizo ni kondomu na mwanamme kumwaga nje shahawa wakati wa tendo la ndoa.
Njia zingine kama majira, kitanzi, vijiti na sindano za depo provera huwa na changamoto ya kuchelewesha upatikanaji wa ujauzito. ( 26, 27, 28 )
Ikiwa unajiandaa kupata ujauzito, na tayari umeshaamua kabisa kuupata, acha kutumia njia hizi ili mwili wako ujiandae.
Usisubiri sana, unaweza kujikuta umechelewa.
11. Tumia dawa
Kuna baadhi ya dawa hutumika katika kuongeza nafasi ya mwanamke kupata ujauzito. Kwa kuwa mimi siyo mganga wa kienyeji basi sitazungumzia upande huo.
Kwa hospitali, baada ya mwanamke kupimwa ikiwa anatatizo lolote la kiafya linalohusu upevushaji wa mayai kuna dawa maalumu huwa zinatolewa.
Kwa wale wenye changamoto za vichocheo, maambukizi au uvimbe wao pia hupatiwa dawa kulingana na changamoto zao.
Mfano wa dawa hizo ni clomiphene citrate, metformin, bromocriptine na letrozole. ( 29, 30, 31, 32, 33 )
Tahadhari kubwa inapaswa katika kutumia dawa hizi, pia zisitumike pasipo kupata ushauri wa wahudumu sahihi wa afya.
Jinsi ya Kupata Mimba Kirahisi
12. Mtindo wa mapenzi
Mbegu za kiume hazihitaji mbwembwe nyingi za mitindo ya kulala kwenye kufanya mapenzi ili ziweze kuogelea vizuri kulifuata yai.
Hata hivyo, mwanamme kulala juu ya mwanamke, mtindo unaofahamika zaidi kama missionary style, pamoja na mwanamme kuingiza uume kutoka nyuma kama mbwa, mtindo maarufu kama doggy style huruhusu uume uzame ndani zaidi.
Hivyo, kwa wanaume wanaotoa mbegu chache hii inaweza kuwa msaada.
Kwa kuwa uume huwa karibu na mlango wa kizazi, mbegu za kiume hazitakuwa na safari kubwa sana ya kuogelea.
Ndani ya dakika chache tu zitaweza kuvuka mlango wa kizazi.
Mtindo wa kufanya mapenzi huku mmesimama, au mwanamke akiwa huu siyo mibaya, lakini kani ya mvutano huwa inafanya kazi kinyume wakati huu.
Haya ni maoni ambayo bado hayajathibitishwa na tafiti za kutosha, hivyo sitakupa uthibitisho wake.
Lakini umeelewa hoja yangu siyo?
Muhtasari
Changamoto za uzazi huhusisha jinsia zote.
Ikiwa mambo haya yatafanyika, lakini changamoto ya kupata ujauzito itaendelea kuwepo, ni muhimu kama wapenzi watafika hospitalini wote kwa pamoja ili wachunguzwe.
Mwanamke kupata hedhi haitoshi kumfanya awe mama, pia mwanamme kufikia mshindo siyo uthibitisho wa kuwa anaweza kumpa mwanamke ujauzito.