Jinsi ya kumsinga Mume
Jinsi ya kumsinga Mume -Neno kusinga linamaanisha kusugua ili kuondoa uchafu.
Ukiona mume ananawiri na ngozi yake ipo laini ujue ni matokeo ya kazi nzuri anayoifanya mkewe nyumbani. Haipendezi mtu mwenye mke kuwa na ngozi ilioparara na kujaa chunusi au nongo. Siku kama ya leo ambayo mume haendi kazini, chukua nafasi hii kumsinga.
Ni vizuri ukamsinga nusu saa baada ya kula chakula cha mchana ili mpate wakati wa kulala au kujamiiana kabla ya swala ya Asr. Hakikisha umejiachia katika mavazi; unaweza kubaki tu na nguo za ndani na kupachika kikuba kwenye nywele ili kuleta mvuto zaidi.
RELATED: Njia za kuongeza wingi wa mbegu za kiume, cheki hapa
Tumia moja kati ya vitu vifuatavyo kumsinga mume wako:
-Mchanganyiko wa unga wa karafuu na liwa
– Unga wa manjano
-Chicha za nazi
– Body scrub zinazouzwa madukani
Jinsi ya kumsinga Mume
Jinsi ya kumsinga Mume
Matayarisho:
-Kwenye bakuli, changanya maji ya mawaridi na majo kati ya vitu vilivyotajwa hapo juu( aidha unga wa karafuu na liwa, unga wa manjano, chicha za nazi au body srub) mpaka iwe kama rojo zito.
– Fukiza leso/khanga gora moja. Moja atalalia mume wakati unamsinga, ya pili atalalia wakati unamkanda. Kumbuka kuchagua leso yenye ujumbe kama uleee tuliozungumzia juzi…
-Mafuta ya nazi, ya ufuta, ya mzaituni au massaging oil kwa ajili ya kumkanda baada ya singo
Jinsi ya kumsinga na kumkanda mume:
-Unaweza kumsinga kitandani, kwenye zulia au kwenye mkeka. Tandika shuka alafu juu yake tandika leso uliyoifukiza. Mume alale shughuli ianze.
– Mpake mchanganyiko uliyotaarisha mwili mzima kasoro sehemu ya siri na macho kwani unga wa karafuu unawasha.
– Msugue mwili mzima kuanzia usoni ukielekea miguuni hususan sehemu zinazokuwa na uchafu kama shingo, nyuma ya masikio, mgongo, makwapa, mbele ya viwiko, kiuno, makalio, mtoki, kinena(kama hutumii unga wa karafuu), katikati ya mapaja, nyuma ya magoti na nyayo mpaka uhisi uchafu na nongo zote zimeisha.
– Kisha mkaoge pamoja mana hapo wewe mwenyewe utakuwa unatokwa na jasho
– Baada ya kuoga, tandika leso ya pili kitandani kwa ajili ya kumkanda
– Unampaka aidha mafuta ya nazi,ya ufuta, ya mzaituni au massaging oil na kuanza kumkanda taratibu na kwa upendo huku ukimnong’oneza maneno ya mapenzi.
– Anza kumkanda kichwa, shingo ukielekea kwenye mabega, mikono, vidole, mgongo, makalio, mapaja, miguu bila kusahau uume wake.
-Akipitiwa na usingizi pumzikeni pamoja. Kama kumkanda kutaleta hisia basi mnaweza hata kufanya tendo la ndoa.
Shughuli hii inasaidia kuondoa uchafu na kupunguza machofu mwilini, inaondoa usongo wa mawazo, huiwezesha mishipa ya damu kuwa katika hali nzuri na hivyo kurahisisha msukumo wa damu mwilini na pia huleta furaha baina ya wanandoa.