Boomplay ni app nambari moja kwa huduma ya kusikiliza na kupakua muziki barani Afrika, inasherehekea Siku Ya Wanawake Duniani 2019 ikiwa na kampeni mpya ya “Boom Queens”.
Vanessa Mdee, Rihanna, Tiwa Savage, Fena Gitu na wengine wengi, ni miongoni mwa wanawake wenye vipaji ambao wameendelea kubadilisha tasnia ya muziki duniani. App ya Boomplay itakuwa na muonekano wa tofauti hasa katika Siku Ya Wanawake duniani tarehe 8 Machi, lengo likiwa ni kuonesha na kukuza kazi za wanawake katika muziki. App itapambwa na nyimbo, albamu pamoja na playlist za wanawake katika vipengele vyote kwenye ukurasa wa kwanza.
Boomplay pia itakuwa na kampeni kabambe ambayo itatoa fursa ya kukuza mauzo ya kazi za wanawake ambao nyimbo zao zitakuwepo kwenye playlist ya BOOM QUEENS. Playlist hiyo itakuwa na nyimbo za wasanii bora wa kike tu.
Katika kampeni hii, Meneja Mahusiano wa kampuni ya Boomplay, Bi Tosin Sorinola amesema, “majadiliano juu ya usawa wa kijinsia ni moja ya mambo ambayo ni muhimu kwetu kama jukwaa lenye nia kubwa ya kukuza wanawake katika muziki, katika njia njema kadri iwezekanavyo. Kampeni hii sio kwa mara moja tu, ni endelevu, na hili litadhihirishwa katika shughuli zetu za kila siku”.
Katika mwezi huu wa kuadhimisha Siku Ya Wanawake Duniani, watumiaji wa Boomplay kupitia simu zao za Android na iOS watapata fursa ya kujishindia simu mpya ya iPhone XS na zawadi nyingine kem kem nchini Tanzania, Kenya, Nigeria na Ghana. Ili kuonesha upendo kwa wasanii wa kike katika tasnia ya muziki, basi jishindie zawadi hizi kwa ku-subscribe kwenye app ya Boomplay kwenye vifurushi vinavyopatikana (vya siku, wiki na mwezi) na pia sikiliza playlist ya Boom Queens.
App ya Boomplay ambayo ina watumiaji zaidi ya milioni 42 dunia kote, hivi karibuni ilizindua app hiyo kwenye jukwaa la iOS. Hakika Boomplay inajivunia kuwa na nyimbo na video zaidi ya milioni 5 kutoka kwa wasanii wa Tanzania na wakimataifa.
Leave a Comment