Promo

DJ DULLY AIBUKA MSHINDI WA SHIDANO LA MDUNDO LA MA-DJ (DJ BATTLE),

DJ DULLY AIBUKA MSHINDI WA SHIDANO LA MDUNDO LA MA-DJ (DJ BATTLE), AKABIDHIWA FEDHA TASLIMU TSH 7,000,000

Desemba 22, 2021: Mdundo, ambayo ni kampuni inayoongoza kwa huduma za muziki mtandaoni Afrika, imemtangaza DJ Dully kuwa ndio mshindi wa mpambano wa Ma-DJ (Mdundo DJ Battle) mwaka huu. Pamoja na ushindi huo, DJ huyo pia amepokea kitita cha Tsh 7,000,000 na muda katika mojawapo ya redio kuonesha uwezo wake live ambapo atacheza DJ mix iliyompa ushindi. Shindano hilo la Ma-DJ liliwavutia zaidi ya washiriki 200.

DJ huyo alikutana na timu ya Mdundo mapema wiki hii ambapo alikabidhiwa hundi yake katika hafla ya aina yake ya kuenzi ushindi huo. Meneja Masoko Mwandamizi, William Abagi alisema, “Shindano hili lilipokewa vizuri na mamia ya Ma-DJ nchi nzima. Tunapenda kutoa shukrani kwa washiriki wote na hasa kwa DJ Dully kwa juhudi za aina yake katika shindano hili.

Shindano hili ni jukwaa maalumu kwa Ma-DJ kutoka Tanzania kuonesha vipaji vyao kwa watumiaji zaidi ya milioni 10 wa Mdundo. Ni moja ya njia za Ma-DJ pia kukuza mashabiki na kupaisha chapa zao ili wafike mbali zaidi na kusikilizwa na watu wengi. Hii ni mara ya kwanza kwa Mdundo kuendesha shindano la aina hii maalumu kwa Ma-DJ.

“Shindano hili limefanikiwa kwa kiasi kikubwa na ni la kwanza la aina hii kuendeshwa na Mdundo kwa kweli tunashukuru muitikio tuliouona. Tunatarajia kuendesha shindano la pili mwakani 2022 na tunatarajia kupata washiriki wengi zaidi kutoka sehemu mbalimbali nchini, alisema Bw. Abagi.

Mdundo inafanya kazi na wasanii zaidi ya 100,000 Afrika na Tanzania ina watumiaji wengi zaidi wa huduma za Mdundo huku ikirekodi watumiaji maalumu milioni 4.1 katika robo ya mwaka kuelekea Septemba 2021.

Mdundo imeshirikiana na Vodacom Tanznaia kuwapa wapenzi wa muziki nafasi ya kupata maudhui yenye hadhi ya Premium-kazi za Ma-DJ (DJ Mixtapes) kwa gharama ya hadi Tsh 100 kwa siku. Kwa tarifa zaidi, mashabiki wa shindano la Mdundo la Ma-DJ  (Mdundo DjJ Battle) wafuatilie  kupitia kurasa za Mdundo za mitandao ya kijamii:  Instagram: @mdundomusicTz , facebook: @mdundomusic, Twitter: @Mdundotanzania.

Mdundo inajivunia zaidi ya watumiaji 10,500,000 kila mwezi kutoka Tanzania, Kenya, Nigeria, Ghana na nchi nyingine Afrika na inafanya kazi na wanamuziki zaidi ya 100,000 Afrika.