Entertainment

Picha Za Mrembo Rita Anayehusishwa na Diamond 

Katika siku za hivi karibuni, mitandao ya kijamii imewaka moto baada ya madai kuibuka kuwa msanii nyota wa Bongo Fleva, Diamond Platnumz, anadaiwa kuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rita Norbeth, mrembo kutoka Afrika Kusini.

Taarifa hizi zilianza kusambaa baada ya Mange Kimambi kuposti kwenye App yake, akidai kuwa Diamond anatoka kimapenzi na Rita Norbeth. Hili limezua taharuki kubwa kwa mashabiki, hasa kwa kuwa inafahamika wazi kuwa Diamond na Zuchu wamekuwa wakihusishwa kimapenzi kwa muda mrefu.

Diamond Platnumz Akanusha Madai Haya

Baada ya tetesi hizi kusambaa, Diamond Platnumz aliamua kuvunja ukimya na kueleza ukweli wake. Kupitia kauli yake, Diamond alikiri kuwa alikuwa na mahusiano na Rita Norbeth tangu mwaka 2023, lakini kwa sasa hawapo tena pamoja. Amefafanua kuwa video zinazotrend mtandaoni zilipostiwa na yeye mwenyewe, lakini kwa sasa hakuna uhusiano wowote kati yao.

Related: Diamond Platnumz – Nitafanyaje

Mashabiki Wapagawa, Zuchu Atema Neno?

Kauli ya Diamond imezua maoni tofauti mitandaoni. Baadhi ya mashabiki wameonyesha hasira na kukosoa kitendo cha Diamond kuhusishwa na mwanamke mwingine huku akiwa na uhusiano na Zuchu. Wengine wanahisi kwamba Mange Kimambi ana lengo la kusambaza drama kwa ajili ya kuwasha moto mitandaoni.

Mpaka sasa, Zuchu hajatoa tamko rasmi kuhusu sakata hili, lakini mashabiki wake wengi wameonyesha kusikitishwa na madai haya, wakidai kuwa yanaweza kuathiri mahusiano yao.

Tazama Picha za Rita Norbeth Hapa

Kwa wale wanaotaka kumfahamu zaidi Rita Norbeth, tazama picha zake hapa

Je, unadhani mahusiano ya Diamond na Zuchu yataendelea kuwa imara baada ya drama hii? Toa maoni yako kwenye sehemu ya comments!

Leave a Comment