LEARNING

Story Za Kusisimua: Siri za Usiku Part 1

Story Za Kusisimua

Nancy, kwani huendi kuhudhuria vipindi leo mwanangu?! Naona umelala mpaka saizi…

Hii ilikuwa sauti ya Aunt yangu, alikuwa ananiamsha ili niende chuo. Mimi naishi na Aunt yangu tu pale nyumbani. Baba yangu aliondoka muda mrefu akisema anatafuta maisha sehemu nyingine, hivyo alimuomba Aunt yangu anilea. Mama yangu aliolewa Kenya na mwanaume mwingine nikiwa primary, hivyo naishi na Aunt yangu kama mtoto wake.

Nililalia hadi saa sita alasiri. Niliona bora niamke ili niweze kumsaidia Aunt yangu na kazi, ingawa tumbo langu la period lilikuwa linaniuma sana. Niliamka, nikashika mopper ili niweze kudeki mule ndani. Hapo Aunt yangu akaingia na kusema, “Mwanangu, nimeshadeki. Ingia bafuni uoge, unywe chai, na mbona umechelewa kuamka? Shida nini?”

“Aunt, naumwa tumbo japo nilikusikia ukiniamsha, lakini nilikuwa usingizini, nikadhani labda naota. Ndiyo maana hata sikuitika,” nikajibu.

Aunt alicheka akasema, “Binti utafikiri mimi sio mtu wa afya, unaumwa lakini husemi?”

“Najua Aunt, lakini ningekuambia, ningekuambia. Wewe ni Baba, Mama na kila kitu kwangu. Nakupenda sana, hakuna kitu naweza kukuficha,” nikamkumbatia na kumkiss. Aunt alifurahi sana.

Aunt yangu ni daktari na anamiliki dispensary yake binafsi huko Kibamboni, lakini tunaishi Tabata, Dar es Salaam. Yeye ni boss katika dispensary hiyo, lakini huwa anakuja tu na madaktari na wauguzi wengine wanakuwapo kwenye huduma.

Mimi nilikuwa nasoma chuo cha DSJ (Dar es Salaam School of Journalism). Siku hiyo nilikaa nyumbani kwa sababu Aunt alinipa dawa za maumivu, hivyo nikaendelea vizuri. Nilikuwa na marafiki wengi lakini sikuwa na mpenzi. Nilikuwa na sababu zangu, lakini rafiki yangu, Pete, alikuwa na wapenzi wengi, lakini hawajui kuhusu kila mmoja.

Siku moja jioni, rafiki yangu (Neema) alinipigia simu na kusema, “Shogaaa, umepataaaa…”

“Mmhh, we nyau, nimepata nini?” nilijiuliza nikiwa na mshangao.

Alikata simu, na nilijaribu kumpigia tena, lakini hakupokea. Nilijaribu tena, lakini hakuinua simu. Niliandika sms kumuuliza, lakini nilikubali kusubiri.

Kisha akatuma sms: “Shogaaa, umepata wale unaowataka. Kuna kaka hapa ni rafiki wa mpenzi wangu, ni daktari na handsome hatariiii 😍.” Rafiki yangu alijua napenda wanaume madaktari na handsome.

Soma: Ibrahim TraorΓ© History

Nilijua kuna jambo linatokea, lakini nilikuwa na mashaka, nikamwambia, “We subiri tu. Nitakuja.”

Muda ulivyokuwa ukizidi kupita, nilikosa kujua nifanye nini. Neema aliniambia tu, “Subiri tu, utafurahi.”

Nilijua inabidi niende, lakini nilikuwa na wazo kuwa Aunt yangu ataniuliza nikirudi nyumbani usiku. Nilimwandikia sms, “Aunt uko wapi, nakupigia simu yako inakata. Mi niko bored, rafiki yangu kaniomba niende kwenye party jirani.”

Aunt yangu aliniamini. Nilijitahidi tu ili nisionekane na wasiwasi. Nilijiandaa kwa kigauni changu kifupi, na kiatu kifupi.

Nilikata Uber na kuelekea kwenye party. Nikiwa pale, nilijaribu tena kumpigia Neema, lakini hakupokea. Nilikuwa nimesimama nje nikisubiri majibu. Ghafla, niliona mrembo mmoja akikuja kwangu akasema, “Hi Miss.”

Nikajibu “Hi too,” kwa kicheko kidogo. Huyu mrembo alikuja kutembea na mimi hadi kwenye ukumbi wa party.

“Samahani kaka, naomba nionane na Neema?” Nilimuuliza.

Yule kaka alicheka na kusema, “Hapana shida, anakuja hivi sasa hivi.”

Alikuwa ananiambia kuwa Neema alikuwa na mpenzi wake na alikuwa akimsubiri.

Muda si mrefu, Neema alionekana na mpenzi wake. Ghafla, nikamwona kijana mwingine nyuma yao, na nilijua ni birthday boy.

Leave a Comment