Mdundo Yaandikisha Idadi Mpya ya Watumiaji Millioni 23.4 Kila Mwezi
Huduma inayoongoza kwa Mziki wa Kiafrika Mdundo.com inasherehekea ushindi mwingine wa kusajili idadi ya watumiaji Milioni 24 katika kipindi cha miezi 3 iliyopita.
Tangu toleo la awali la umma(IPO) la 2020, huduma hiyo imekuwa na ushirikiano wa kampuni za mitandandao ya simu ambazo zimefanikisha ukuaji wa bidhaa ya kipekee; DJ Mixes. Mdundo pia imebadilisha matoleo yake ya bidhaa, kwa kuongeza maudhui ya burudani mtandaoni ili kuangazia maudhui kama vile maoni ya soka,simulizi za kidini, podikasti na zinginezo.
Mdundo DJ Mixes ni huduma ya muziki ya kipekee ambayo huwapa watumiaji uwezo wa kupakua na kuskiza DJ mixes zilizoratibiwa kwa kipekee; huku zikifanyiwa mabadiliko mara kwa mara kila wiki. Hizi ni mixes ambazo utazipata kupitia watoa huduma za mawasiliano ya simu kama vifurushi vya muziki. Mixtapes na mixes za Mdundo zinapatikana katika takriban aina zote za muziki za Kiafrika kama vile Afrobeat, Bongo, Gospel, Amapiano, Afropop, Highlife na Hiplife. Aina za muziki za kiasili au utamaduni kama vile Kihausa na Singeli zinapatikana pia.
‘Timu ya Mdundo imebadilisha kabisa ukubwa wa biashara yetu katika robo 10 zilizopita tangu IPO yetu. Kama timu, wamefanya maamuzi magumu. Timu inapatana na changamoto mbali mbaliĀ kila mara na wadau wa nje, wawekezaji, wajumbe wa bodi na mimi mwenyewe juu ya maamuzi wanayofanya na jinsi wanavyotanguliza muda na rasilimali zao.’ aliandika Mkurugenzi Mtendaji wa Mdundo Martin Nielsen kwenye LinkedIn.
Uchanganuzi wa haraka wa taswira ya maarifa kama yalivyoshirikiwa mapema leo:
Mdundo iliandikisha watumiaji milioni 23.4 wanaotumia kila mwezi (MAU) mnamo Desemba 2022 huku nchi 6 zikisajili Milioni 1 na zaidi.
Huduma ya kulipia ilizinduliwa na MTN nchini Afrika Kusini. Hii sasa inapatikana katika masoko 4 muhimu; Tanzania, Nigeria, Ghana na Afrika Kusini.
Mdundo inajivunia kufikia Milioni 49 kila robo mwaka kwa watangazaji wa wakuu wa biashara barani Afrika kwenye huduma hiyo.
Mdundo iliongeza orodha ya nyimbo bora kwenye jukwaa lake kwa kutumia ushirikiano muhimu na washirika wa Utoaji Leseni kote Afrika.
Mafanikio yote yanaambatana na lengo la Mdundo la mwaka 2025 la kufikia watumiaji milioni 50 wanaotumia kila mwezi na thamani ya kufikia malengo kwa kila mtumiaji kupitia bidhaa bora za mawasiliano ya simu.
Wanachama na marafiki wa Mdundo wameeleza kufurahishwa kwa maendeleo yanayoshuhudiwa. Kwa pamoja wanafurahia maendeleo ya baadae yatakayoafikiwa na Mdundo.