Tanzanian music giant Diamond Platnumz has officially released the heartfelt lyrics for his latest song, Moyo. This emotional track speaks about perseverance, struggles, and faith in the journey of life.
If you’re looking for the full lyrics to sing along while listening to the song, you’re in the right place. Scroll down to read the lyrics and enjoy the music!
Diamond Platnumz – Moyo Lyrics
Verse 1
Pole pole pole,
Pole pole,
Moyo wangu,
Masikini pole,
Pole mtima wangu.
Haikuwa dhamira,
Haikuwa kusudi langu,
Haikuwa dhumuni waala,
Haikuwa malengo yangu.
Ila tuseme,
Labda moyo,
Pengine sio,
Ridhiki.
Maana,
Nimejitahidi sana,
Malengo hayafiki.
Kama kuswali,
Naswali sana,
Mpaka sunna za usiku.
Kazi nimetafuta sana,
Ila siambulii kitu.
Sitaki kukufuru Mungu,
Sababu najua ni mapito.
Japo inakatisha tamaa,
Ila siku yangu ipo.
Chorus
Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.
Moyo wangu, moyo,
Usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.
(Instrumental)
Verse 2
Penzi maua,
Pesa mbolea.
Hata shemeji yako,
Ana mengi ila,
Hawezi ongea.
Moyo,
Najitahidi jiepusha vya watu,
Ni majaribu aah,
Japo nna shida,
Ila naepuka tamaa.
Moyo,
Nlitamani siku moja,
Na mimi nimjengee mama,
Ila ndo vile tu umasikini,
Mipango inakwama.
Hua naumia,
Watoto shuleni,
Wakifukuzwa ada.
Najiona mjinga,
Yani sio bora baba.
Sitaki kukufuru Mungu,
Najua ni mapito.
Maana riziki mafungu,
Nami langu siku lipo.
Chorus
Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.
Moyo, usiumie,
Moyooo, ni mapito,
Ohh moyo,
Haya yote,
Mitihani na yana mwisho.
(Instrumental fade out…)
Download Diamond Platnumz – Moyo
Want to download this song? Click here to get it now and enjoy Diamond Platnumz’s powerful vocals and deep lyrics!
What do you think about this song? Drop your thoughts in the comments!
Leave a Comment