Sheria Katika Lugha Rahisi
Kimetolewa na Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara
Juni, 2015
KIMEANDALIWA NA
Kamati ya Utafiti na Machapisho ya Chama Cha Wanasheria Tanganyika
Wajumbe:
- Cyriacus Binamungu (Mwenyekiti)
- Daniel Welwel (Mjumbe)
- Madeline Kimei (Mjumbe)
- Alex Makulilo (Mjumbe)
- Ally Possi (Mjumbe)
- Lilian Mongella (Mjumbe)
- Frank Mirindo (Mjumbe)
- Elifuraha Laitaika (Mjumbe)
- Judith S. Kapinga (Katibu wa Kamati)
Waratibu:
- Seleman Pingoni
- Kaleb Gamaya (CEO-TLS)
- TEPHEN mSECHU (PO-RPA)
- Selemani Pingoni (M & E Officer)
HAKIMILIKI 2015 TLS
Kijarida hiki ni mali ya Chama cha Wanasheria Tanzania Bara na ni kosa kurudufu au kuchapa au kutumia kwa namna yoyote itakayokuwa kinyume na hakimiliki ya Chama Cha Wanasheria bila idhini au ruhusa ya maandishi ya Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara.
SHUKRANI
Kamati ya Utafiti na Machapisho ya Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara kwa niaba ya Baraza la Uongozi la Chama inatoa shukrani za dhati kwa wadau wote na wanachama wa Chama Cha Wanasheria Tanzania Bara kwa kushiriki kikamilifu katika hatua mbalimbali za kuandaa kijarida hiki.
Kwa namna ya pekee, Kamati inapenda kuishukuru pia Sekretariati ya chama kwa kazi kubwa walioifanya na inashukuru wanachama wa Chama Cha Wanasheria kwa ushirikiano wanaoendelea kutoa katika kufanikisha kazi za chama.
UTANGULIZI
Chama Cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Law Society) ni chama kilichoanzishwa na Sheria ya Bunge ya 1954 Sura Na.307. Kwa mujibu wa sheria hiyo, Chama kinawajibu wa kuisaidia serikali katika masuala yahusuyo sheria na pia kuieleimisha jamii kisheria katika kupata haki zao za msingi.
Katika kutimiza jukumu lake kwa wanajamii Chama Cha Sheria Tanganyika kimeandaa kijarida hiki cha sheria katika lugha rahisi kiitwacho “IJUE SHERIA YA ARDHI NA TARATIBU ZINAZOHUSIKA KUPATA, KUMILIKI NA KUUZA ARDHI VIJIJINI NA MJINI’’.
Kijarida hiki kimeandaliwa kwa lengo la kujenga uwezo wa wanajamii katika kufahamu taratibu za umiliki wa ardhi na matumizi bora ya ardhi kwa mujibu wa sheria za ardhi Tanzania. Kijarida hiki kimeelezea kwa kina kuhusu maana ya ardhi, misingi mikuu ya ardhi kitaifa, mgawanyo wa ardhi nchini Tanzania, utawala na mamlaka za ardhi nchini Tanzania, aina za umiliki wa ardhi nchini Tanzania, taratibu za kuomba umiliki wa ardhi Tanzania, haki za wanawake katika kumiliki ardhi, haki za wafugaji katika matumizi ya ardhi na matumizi bora ya ardhi.
YALIYOMO
- Maana ya Ardhi
- Upatikanaji wa Ardhi Tanzania
- Upatikanaji na Umiliki wa Ardhi Tanzania
- Haki Miliki
- Maombi ya Kumiliki Ardhi ya Kijiji
- Sifa za Haki Miliki ya Kimila
- Haki za Wafugaji Katika Matumizi ya Ardhi ya Kijiji
- Haki za Wanawake katika Ardhi
- Mauzo katika Ardhi chini ya Hati Miliki ya Kiserikali
- Rehani Katika Ardhi
- Mauzo katika Ardhi ya Kijiji chini ya Hati Miliki ya Kimila
- Taratibu za Kufuata ili Kupata Mkopo kwa Kuweka Ardhi Rehani
- Matokeo ya Kushindwa Kulipa Mkopo
- Taratibu za Kukomboa Fedha Endapo Mweka Rehani Atashindwa Kulipa Mkopo
- Fidia ya Ardhi
- Utatuzi wa Migogoro ya Ardhi
- Baraza la ardhi la kijiji
- Baraza la Kata
- Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya na Mamlaka ya Baraza la Ardhi na Nyumba la Wilaya
- Rufaa Kutoka Baraza la Ardhi na Nyumba
- Mahakama Kuu na Mahakama Kuu
- Mahakama ya Rufani
Unaweza Soma: Mikopo Ya Halmashauri Kwa Vijana 2025
SEHEMU YA 1: Dhana na Maana ya Ardhi
Ufafanuzi
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwahi kunukuliwa akisema kwamba, ili tuendelee tunahitaji vitu vinne katika kuchangia maendeleo. Vitu hivyo ni Ardhi, Siasa Safi, Uongozi Bora na Watu. Kwa msingi huu Mwalimu alimaanisha kwamba, ardhi ni miongoni mwa misingi madhubuti ya Maendeleo.
Maana ya Ardhi
Ardhi ni sehemu yote iliyo juu na chini ya uso wa nchi, vitu vyote vyenye kuota kiasili juu ya nchi, majengo na miundo mingineyo iliyokaziwa kwa kudumu juu ya ardhi.
Angalizo: Petroli na aina zote za madini zinazopatikana chini ya ardhi sio sehemu ya ardhi.
Misingi Mikuu ya Ardhi Kitaifa
- Ardhi yote ni mali ya umma na imekabidhiwa kwa Raisi kama mdhamini (msimamizi) mkuu kwa niaba ya watanzania wote;
- Kulinda haki zote za miliki za ardhi zilizopo, yaani miliki ya ardhi ya kimila na ile ya kiserikali;
- Kugawa ardhi kwa haki na kwa raia wote wa Tanzania;
- Kudhibiti kiasi ambacho mtu mmoja au taasisi yaweza kumiliki na kutumia kwa mahitaji yake bila kuwaathiri Watanzania au wanajamii wengine;
- Kuwezesha utumiaji endelevu wa ardhi katika shughuli za kiuzalishaji kwa manufaa ya wote;
- Kuhakikisha kwamba maslahi yeyote katika ardhi yana thamani na yanalindwa katika muda wowote wakati wa mapatano yanayoweza kuathiri thamani ya mmiliki;
- Kulipa fidia kamili na kwa wakati kwa mtu yeyote ambaye haki miliki ya ardhi yake inafutwa, inabadilishwa au inaingiliwa kwa namna yeyote na serikali kwa manufaa ya umma na yeye kuathirika na zoezi hilo;
- Kuweka mfumo thabiti, wa wazi na rahisi katika kusimamia ardhi;
- Kuwawezesha raia wote kushiriki katika kutoa maamuzi ya mambo yanayohusiana na miliki na matumizi yako ya ardhi;
- Kuwezesha uendeshaji wa bora wa soko la ardhi;
- Kulinda haki za wakulima na wafugaji wadogo vijijini na mijini kwa kudhibiti matumizi ya ardhi;
- Kuweka kanuni za sheria za ardhi ambazo zinapatikana kwa urahisi na zinazoeleweka kwa raia wote;
- Kuwezesha kuwepo kwa mfumo huru, rahisi na unaofanya kazi kwa haraka katika suala zima la utatuzi wa migogoro ya ardhi;
- Kutoa haki sawa kwa jinsia zote (mwanamke na mwanaume) kumiliki, kutumia na kufanya shughuli yeyote kwenye ardhi bila kuweka mipaka yeyote; na
- Kuhimiza usambazaji wa taarifa zozote zinazohusu ardhi kwa raia wote wa Tanzania.
Soma Zaidi Hapa Chini:
Leave a Comment