Wanafunzi 149,818, ambao ni sawa na asilimia 69.96, wamechaguliwa rasmi kujiunga na masomo ya kidato cha tano kwa mwaka wa masomo 2025. Wakati huo huo, wanafunzi 64,323 wamechaguliwa kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu, ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha nguvu kazi yenye ujuzi nchini Tanzania.
Kwa mujibu wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa Mohamed Mchengerwa, jumla ya wanafunzi 214,141 (wasichana 97,517 na wavulana 116,624) walibainika kuwa na sifa stahiki za kujiunga na masomo ya kidato cha tano na vyuo mbalimbali vya elimu ya ufundi. Miongoni mwao, wanafunzi 1,028 ni wale wenye mahitaji maalumu, waliopata nafasi hiyo maalumu kwa kuzingatia mazingira yao ya kielimu.
Mheshimiwa Mchengerwa alitoa taarifa hii muhimu leo Juni 6, 2025, akielezea mafanikio ya serikali katika kuratibu uchaguzi wa wanafunzi wanaoendelea na elimu ya juu ya sekondari na mafunzo ya ufundi. Alieleza kuwa mchakato wa uchaguzi umezingatia vigezo vya kitaaluma na usawa wa kijinsia, ili kuhakikisha vijana wote wenye sifa wanapata fursa ya kuendelea na masomo.
Related: Majina ya wanafunzi na shule walizopangiwa 2022/2023
Jinsi ya Kuangalia Majina ya Waliochaguliwa:
Orodha kamili ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha tano, pamoja na fomu za kujiunga na vyuo vya elimu ya ufundi na ualimu kwa mwaka 2025, inapatikana katika tovuti rasmi zifuatazo:
🔹 Ofisi ya Rais – TAMISEMI: www.tamisemi.go.tz
🔹 Baraza la Taifa la Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET): www.nactvet.go.tz
Au Bofya Hapa Kutazama Orodha Ya Wanafunzi Waliochaguliwa Kujiunga Na Kidato Cha Tano.
Wazazi, walezi, na wanafunzi wote wanahimizwa kutembelea tovuti hizo ili kupata taarifa rasmi na kufanya maandalizi muhimu kabla ya tarehe ya kuripoti.
Beka Boy itaendelea kukuletea taarifa zote muhimu kuhusu matokeo, uchaguzi wa wanafunzi, elimu ya sekondari, vyuo vya ufundi na masuala yote yanayohusu maendeleo ya elimu Tanzania.
Tembelea bekaboy.com kila siku kwa taarifa za uhakika na zinazotrend!
Leave a Comment