Lyrics

D Voice Ft Zuchu – Baby Mpya Lyrics

D Voice Ft Zuchu - Baby Mpya Lyrics

Wapenzi wa muziki wa Bongo Fleva, D Voice kwa kushirikiana na mrembo wa Bongo Zuchu, wametuletea kibao kipya chenye mahadhi ya kuvutia kinachoitwa “Baby Mpya”. Huu ni wimbo wa mapenzi unaosheheni mahadhi ya sebene na ujumbe mzito, unaovutia kila mpenzi wa muziki wa kizazi kipya.

Katika makala hii, tumekuandalia maneno kamili (lyrics) ya wimbo huu kwa mpangilio mzuri ili uweze kuusikiliza huku unasoma kwa wakati mmoja, jambo litakalokusaidia kuuelewa na kuupenda zaidi wimbo huu mpya wa moto!

Pakua wimbo hapa D Voice Ft Zuchu – Baby Mpya

Lyrics: D Voice Ft Zuchu – Baby Mpya

ZUCHU (Intro & Verse):
Alokwambia kahadithiwa,
Na aliyehadithiwa kakosea kukwambia,
Na aliyemwambia alihadithiwa,
Na yeye akakosea kumwambia.

Wala sijafubaa,
Tena sikuhizi nimezidi utundu,
Nashukuru mashallah rangi kama mzungu,
Niliyempata kichaa nampa mpakaa aaah,

Ndani sebene sebene,
Hadi raha…

Chorus (Zuchu):

Sasa ya nini nifiche fiche,
Baby mpya mtamu,
Mimi mwenzenu siwezi kuficha,
Baby mpya mtamu.

Ya nini nijibane bane,
Baby mpya mtamu,
Mimi mwenzenu siwezi kuficha,
Baby mpya mtamu.

Verse 2 – D Voice:

Na nilikua na kusitiri tu,
Maana nisikufiche we ni mbaya sana,
Mi nashukuru tulivyoachana,
Kurudiana tutaongopeana.

Naona unakazana,
Kushindana na walokuzidi,
Huyu mwenzako king anakuongoza ligi,
Utamaliza vioo kujiseti mawigi.

Nishavuka levo hizo,
Sitembei na ma bibi,
Sijafubaa tena sikuhizi nimezidi utundu,
Nashukuru mashallah, rangi kama mzungu,
Nilompata kichaa anipa mpakaa,

Ndani sebene sebene, hadi raha…

Chorus (Zuchu):

Sasa ya nini nifiche fiche,
Baby mpya mtamu,
Mimi mwenzenu siwezi kuficha,
Baby mpya mtamu.

Ya nini nijibane bane,
Baby mpya mtamu,
Mimi mwenzenu siwezi kuficha,
Baby mpya mtamu.

Bridge & Outro (D Voice & Zuchu):

Wekaa ayaa sasa ya leo kali mama,
Ya leo kali dada,
Ya leo kali dada,

Mama kafanyaje huyo?
Kapostiwa usoni amewekwa stika,
Kafanyaje huyo?
Kaenda kudanga, karudi kaachika.

Kafanyaaje?
Amenunua iPhone tandika,
Kafanyaje?
Kaambiwa ukweni hajulikani.

Haya usimuone anatetemeka, anaandida huyo,
Usimuone anarukaruka, anaandida.
Masela usimuone anatetemeka, ana andida huyo,
Msimuone anaruka ruka, ana andida.

Misifa mingine bhana,
We wala hainogi,
Misifa mingine bhana,
We wala hainogi.

Eti nikuongee simu halafu nadaiwa kodi?
Oyaa wee unaota eeh,
We nenda ukalale,
Kama nikikuhonga kweli,
Niite mbwa niko pale.

Oyaa wee unaota eeh,
We nenda ukalale,
Kama nikikuhonga kweli,
Niite mbwa niko pale.

Haya haukatazwi kulilia mapenzi mama Dullah,
Haukatazwi kulilia mapenzi mama Dullah.

Swali la msingi, ila kwanza umekula,
Swali la msingi, shoga kwanza umekula.
Haukatazwi kulilia mapenzi mama Dullah,
Ila swali la msingi, shoga kwanza umekula,
Swali la msingi, udugu kwanza umekula…

Acha… Aaaaaha… Aaaaahha… Veri gudiii!

Pakua wimbo sasa hivi kwa kubofya hapa:

D Voice Ft Zuchu – Baby Mpya | Download MP3

Leave a Comment