Entertainment

Haji Manara Kuachia Wimbo wa ‘Ramadhan’

Haji Manara Kuachia Wimbo wa ‘Ramadhan’

Mwanahabari na mhamasishaji maarufu wa michezo, Haji Manara, ametangaza kuachia wimbo wake mpya wa Qaswida uitwao Ramadhan, ambao ni maalum kwa mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

Kupitia akaunti yake ya Instagram, Haji Manara aliwajulisha mashabiki wake juu ya ujio wa wimbo huu kwa maneno yafuatayo:

“Niliahidi ndani ya Ramadhani hii kutoa na kuimba Qaswida (Nyimbo) maalum ya mwezi huu mtukufu. Alhamdulillah jana mimi na vijana wangu ambao ni mabingwa kwenye hizi kazi, tulikamilisha kazi ya kurekodi na kesho Insha’Allah tutaichia mchana.”

Related: Haji Manara and Zaiylissa Tie the Knot, Dulla Makabila Raises Accusations

Ujumbe wa Wimbo ‘Ramadhan’

Wimbo huu unalenga kuhamasisha waumini wa Kiislamu kuzingatia ibada, dua, na matendo mema katika kipindi hiki muhimu cha Ramadhani. Pia, unasisitiza fadhila za mwezi huu mtukufu na umuhimu wa kumcha Mwenyezi Mungu.

Rekodi na Utoaji wa Wimbo

Kwa mujibu wa Manara, wimbo Ramadhan ulirekodiwa kwa umakini mkubwa, na tayari umerikodiwa rasmi kama alivyoahidi. Alihitimisha ujumbe wake kwa kusema:

“Kaa standby kusikiliza Karma nyingine za Waja wa Mungu, Vocco kweli zinakuja kutoa onyo sahihi.”

Mahali pa Kusikiliza

Mashabiki wanaweza kusikiliza na kupakua wimbo huu mpya kwenye majukwaa mbalimbali ya muziki. Endelea kufuatilia Bekaboy kwa taarifa zaidi kuhusu nyimbo mpya na matukio ya burudani!

Leave a Comment