MUSIC AUDIO

Yesu Kwetu Ni Rafiki – Tenzi za Rohoni Na. 9

Yesu Kwetu Ni Rafiki – Tenzi za Rohoni Na. 9

Yesu Kwetu Ni Rafiki ni moja ya tenzi maarufu kutoka Tenzi za Rohoni, tenzi namba 9. Wimbo huu unasisitiza umuhimu wa kumtumaini Yesu katika maombi, kwani Yeye ndiye rafiki wa kweli anayesikia na kujibu sala zetu.

Maneno ya Wimbo:

1.

Yesu kwetu ni rafiki,
Huwamiwa haja pia;
Tukiomba kwa Babaye,
Maombi asikia;
Lakini twajikosesha,
Twajitweka vibaya;
Kwamba tulimwomba Mungu,
Dua angesikia.

2.

Una dhiki na maonjo?
Una mashaka pia?
Haifai kufa moyo,
Dua atasikia;
Hakuna mwingine mwema,
Wa kutuhurumia;
Atujua tu dhaifu,
Maombi asikia.

3.

Je, hunayo hata nguvu,
Huwezi kuendelea?
Ujapodharauliwa,
Ujaporushwa pia?
Watu wange kudharau,
Wapendao dunia;
Hukwambata mikononi,
Dua atasikia.

Related: Yesu Kwetu Ni Rafiki Mp3 Download

Wimbo huu ni faraja kwa waumini wote, ukikumbusha kuwa Yesu ni rafiki mwaminifu ambaye yuko tayari kutusikia na kutufariji katika kila hali. Basi, tumuombe bila kukata tamaa, kwani Yeye husikia maombi yetu!

Leave a Comment