Lyrics

Vanillah – Ni Kwa Muda Lyrics

Vanillah – Ni Kwa Muda Lyrics

Tanzanian Bongo Flava sensation Vanillah has officially released the lyrics for his emotional hit song, Ni Kwa Muda. This heartfelt track explores the struggles of love, heartbreak, and resilience, making it relatable to many fans. If you’ve been searching for the full lyrics to sing along while listening to the song, you’re in the right place!

Download “Ni Kwa Muda” by Vanillah HERE

Now, let’s dive into the lyrics and experience the deep emotions in this song.

Vanillah – Ni Kwa Muda Lyrics

Mmmmmmh Mhhhhh Mhhh!
Ma Feeling Records

[Verse 1]
Najua mi sio rangi
Uipendayo
Ila naeza
Nikapendezesha
Mchoro wako

Na sina sura nzuri
Ya kuringia
Ila naeza
Kuilinda na
Kuitunza heshima yako

Kwa juhudi za mambo
Hayo unayofanya baby
Hivi unalipwa na nani
Au tuseme pengine
Umeamua maybe
Kumsaidia shetani

Nilifurahi kuona
Umezaliwa na macho
Ila naumia kuona huoni
Nikajitolea hata
Kuumia kwa ajili yako
Hukunipa pole
Pale sikomi

Asante
Asante ya punda
Kweli ni matake
Niachee
Yee niteseke
Niuvue huu upweke

[Pre-Chorus]
Binadamu tuliumbwa
Na madhaifu ndo maana
Hujanipiga ile ngumi ya ndani

Hongera kwa maumivu
Unayonipa mimi
Japo unajifanya huoni

[Chorus]
Ila ni kwa muda tu
Pamoja na maumivu
Yote nayopita
Kwenye mapenzi
Ni kwa muda tu

Haya hayatodumu kwangu
Najua kwamba
Ni kwa muda tu

Mateso unayonipa mi
Nakonda kisa mapenzi
Ni kwa muda tu

Sikuumbwa niwe hivi mi
Nizeeshwe na mapenzi
Ni kwa muda tu

Kwa mudaa, kwa muda, kwa mudaa
Kwa muda


[Verse 2]
Wewe huna huruma
Hata kwa mama aliyenizaa
Anapata presha kuona
Umeniyumbisha kabisa

Hata picha zangu za nyuma
Naona kama zinanizomea
Nilivyokuwa nimenona
Now nimebaki mifupa

Na siwezi kukulaani
Japo amani yangu
Na furaha umevichukua

Ni zaidi ya mateso
Hata adui yangu
Siwezi kumuombea yaliyonikuta

Mapenzi shoti ya umeme
Umesahau tulivyo bang bang
Kwanini umenidharau baby
Bado siamini unanifanya nilie

[Chorus]
Ila ni kwa muda tu
Pamoja na maumivu
Yote nayopita
Kwenye mapenzi
Ni kwa muda tu

Haya hayatodumu kwangu
Najua kwamba
Ni kwa muda tu

Mateso unayonipa mi
Nakonda kisa mapenzi
Ni kwa muda tu

Sikuumbwa niwe hivi mi
Nizeeshwe na mapenzi
Ni kwa muda tu

Kwa mudaa, kwa muda, kwa mudaa
Kwa muda, ni kwa muda tu

Listen & Feel the Music

The lyrics of Ni Kwa Muda tell a powerful story of love, pain, and hope. If you haven’t listened to the song yet, download it now HERE and sing along!

Stay tuned to Bekaboy for the latest music updates, lyrics, and entertainment news!

Leave a Comment