Mwanamitindo maarufu na mfanyabiashara, Hamisa Mobetto, pamoja na kiungo mahiri wa Yanga SC, Stephane Aziz Ki, wanatarajia kufunga ndoa rasmi mwaka huu. Kupitia mitandao yao ya kijamii, wawili hawa wameweka wazi tarehe muhimu za harusi yao, jambo ambalo limeibua hisia kubwa kwa mashabiki wao.
Tarehe Rasmi za Harusi ya Hamisa Mobetto na Aziz Ki
Wapenzi hawa wameshare ratiba rasmi ya harusi yao kupitia mtandao wa Instagram, ambapo wameeleza kuwa:
- Mahari Day: 15 Februari 2025
- Nikkah Day: 16 Februari 2025
- Celebration Day: 19 Februari 2025
Sherehe hizi zote zitafanyika kwa heshima kubwa na zitakuwa LIVE kupitia Zamaradi TV, Channel namba 413 AZAM. Mashabiki na wapenzi wa wanandoa hawa wanatarajia kuona tukio hili la kihistoria likifanyika kwa shangwe na nderemo.
Aziz Ki Amwaga Povu la Mapenzi kwa Hamisa Mobetto
Katika siku ya wapendanao (Valentine’s Day), Aziz Ki alitumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea hisia zake za dhati kwa mpenzi wake Hamisa Mobetto. Maneno yake yaliwagusa wengi na kuonesha ni kwa kiasi gani anathamini uhusiano wao. Aliandika:
“As a footballer, my life is shaped by big decisions—moves, shots, and choices that define my journey. But one decision I’ve never questioned, not even for a second, is choosing you.
From the moment I met you, I knew you were my forever. With you, there is no fall—only flight. You are my greatest victory, my most beautiful dream come true.
Last year, I took the most important shot—not on the pitch, but on one knee. And when you said YES, my world changed forever.
Nakupenda sana, Hamisa. Thank you for choosing me, for loving me, for walking this journey with me.”
Hamisa Mobetto Amjibu kwa Maneno Matamu
Hamisa Mobetto naye hakusita kuonesha mapenzi yake kwa Aziz Ki kwa kumjibu kwa maneno yenye hisia kali, akionyesha furaha yake kwa hatua kubwa wanayopiga katika maisha yao ya kimapenzi. Kupitia Instagram, aliandika:
“A thousand yes to you my love Aziz Ki!
Happy Valentine’s to you my love. GOD knew my heart needed you.
Ahsante kwa kuwa mwanaume mwenye msimamo juu yangu, hii ndiyo mara ya kwanza nina experience hii kwenye maisha yangu.
Nikiongea sana naweza nisimalize leo ila 🙌🏽
Thank you for being the man of your words 🥹
GOD knew my heart needed you & Nina mshukuru Mungu kila leo kwa ajili yako.”
Related: Dady Master (Mb Dogg) Ft Hamisa Mobetto – Sawasawa
Mashabiki Wafurahia Mapenzi ya Aziz Ki na Hamisa Mobetto
Wapenzi wa mastaa hawa wamefurahia taarifa za ndoa na wameonyesha sapoti kubwa kupitia mitandao ya kijamii. Hashtags kama #HamisaMobetto #AzizKi #Wedding2025 zimekuwa zikitrend huku wengi wakisubiri kwa hamu kuona namna harusi yao itakavyokuwa ya kifahari.
Kwa mashabiki wote wa Hamisa na Aziz Ki, hakikisheni hamkosi kushuhudia tukio hili LIVE kupitia Zamaradi TV, Channel 413 AZAM. Harusi hii inatarajiwa kuwa moja ya sherehe kubwa zaidi za mastaa nchini Tanzania mwaka 2025!
Leave a Comment