Habari njema kwa watahiniwa wote wa kujitegemea na wanafunzi wa shule kwa mwaka wa masomo wa 2025! Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) limefungua rasmi dirisha la usajili wa mitihani ya kitaifa. Huu ni wakati muhimu kuhakikisha unajisajili mapema ili kuepuka changamoto za malipo ya ada ya ziada (penalty).
Muda wa Usajili
Kwa wale wote wanaotaka kujisajili, kipindi cha usajili bila penalty ni hadi mwishoni mwa Februari 2025. Baada ya hapo, usajili utaendelea lakini kwa gharama ya penalty kuanzia Machi 2025.
Njia za Kufanya Usajili
NECTA imeweka njia rahisi za usajili kwa watahiniwa, iwe wewe ni mwanafunzi wa kujitegemea au unayetoka shule za private.
- Usajili Mtandaoni
- Tembelea tovuti rasmi ya NECTA kupitia necta.go.tz.
- Fuata hatua zilizoelekezwa na ukamilishe usajili wako popote ulipo.
- Usajili kupitia Posta
- Unaweza pia kutembelea ofisi za Posta zilizo karibu nawe kwa msaada wa kusajiliwa.
Mahitaji Muhimu kwa Usajili
Kabla ya kuanza mchakato wa usajili, hakikisha una reference number, ambazo hutolewa na vituo maalum vya kufanyia mitihani. Hii ni muhimu kwa ajili ya kukamilisha hatua zote za usajili.
Mabadiliko ya Mfumo wa Mitihani kwa QT
Kuanzia mwaka 2024, Baraza la Mitihani lilifanya mabadiliko makubwa kwenye mfumo wa mitihani kwa watahiniwa wa kujitegemea waliokuwa wakijulikana kama QT (Qualifying Test). Sasa watahiniwa hawa:
- Wanaitwa Private Candidates (PC).
- Watafanya mitihani sawa na ile inayofanywa na wanafunzi wa shule (School Candidates).
Hii inaleta usawa na uwiano wa mitihani kwa wote, bila kujali kama ni wanafunzi wa shule au watahiniwa wa kujitegemea.
Hitimisho
Usikose fursa hii ya kujisajili mapema! Hakikisha unakamilisha usajili wako ndani ya muda uliopangwa ili kuepuka adhabu ya malipo ya ziada. Kwa maelezo zaidi, tembelea tovuti rasmi ya NECTA au fika kwenye ofisi za Posta kwa msaada zaidi.
Soma tangazo hapa kwa taarifa muhimu kama hizi na habari nyingine zinazohusu usajili.
Leave a Comment