Serikali imeendelea kuchukua hatua za kuhamia mifumo ya kidigitali ili kupunguza matumizi ya karatasi na kuboresha ufanisi wa kazi. Wakati huo huo, benki mbalimbali zimekuwa zikijitahidi kuboresha hali ya maisha ya watumishi kupitia huduma za mikopo.
Sasa zile enzi ambapo mwalimu alilazimika kusaga na lumba akitembelea benki kuulizia habari za mikopo, kujaza fomu nyingi, kisha kuzipeleka kwa maafisa utumishi kwa uthibitisho, zimebaki historia. Mfumo wa ESS umekuwa suluhisho, ukirahisisha mchakato mzima wa kuomba mikopo kwa watumishi wa umma.
Kwa mfumo huu wa ESS, mtumishi wa umma anaweza kuchagua benki au taasisi ya fedha anayotaka kukopa bila usumbufu. Hadi sasa, taasisi nane za kifedha zimejiunga na mfumo huu, zikitoa fursa mbalimbali kwa waombaji mikopo.
Mfano wa Taasisi za Fedha na Mikopo Yao
Hapa kuna baadhi ya taasisi za fedha zinazotoa mikopo kwa watumishi wa umma kupitia mfumo wa ESS:
1. Exim Bank
- Aina ya Mkopo: Wafanyakazi Loan
- Kiwango cha Juu: 200,000,000
- Kiwango cha Chini: 200,000
- Bima: 0.5%
- Muda wa Kulipa: Miezi 3 – 120
- Riba: 13%
2. DTB Bank
- Aina ya Mkopo: Rafiki Loan
- Kiwango cha Juu: 150,000,000
- Kiwango cha Chini: 1,000,000
- Bima: 0.55%
- Muda wa Kulipa: Miezi 6 – 108
- Riba: 16%
3. CRDB
- Aina ya Mkopo: Mkopo wa Mfanyakazi
- Kiwango cha Juu: 200,000,000
- Kiwango cha Chini: 100,000
- Bima: 0.75%
- Muda wa Kulipa: Miezi 12 – 108
- Riba: 16%
4. Azania Bank
- Aina ya Mkopo: Consumer Loan
- Kiwango cha Juu: 150,000,000
- Kiwango cha Chini: 200,000
- Bima: 0.4%
- Muda wa Kulipa: Miezi 3 – 96
- Riba: 14%
5. Letshego Bank
- Aina ya Mkopo: Faidika Watumishi Loan
- Kiwango cha Juu: 70,000,000
- Kiwango cha Chini: 200,000
- Bima: Hakuna
- Muda wa Kulipa: Miezi 6 – 96
- Riba: 36%
6. TCB Bank
- Aina ya Mkopo: Consumer Loan
- Kiwango cha Juu: 300,000,000
- Kiwango cha Chini: 500,000
- Bima: 1%
- Muda wa Kulipa: Miezi 6 – 108
- Riba: 16%
7. NMB
- Aina ya Mkopo: Mkopo wa Mfanyakazi
- Kiwango cha Juu: 200,000,000
- Kiwango cha Chini: 200,000
- Bima: 0.75%
- Muda wa Kulipa: Miezi 2 – 120
- Riba: 17%
8. NBC
- Aina ya Mkopo: Mkopo wa Mshahara
- Kiwango cha Juu: 200,000,000
- Kiwango cha Chini: 100,000
- Bima: 0.75%
- Muda wa Kulipa: Miezi 12 – 108
- Riba: 18%
Related: Jinsi ya Kuingiza Majukumu (Tasks na Subtasks) Kwenye Mfumo wa ESS
Kwa mtazamo huu mpya, watumishi wa umma wana nafasi ya kulinganisha masharti na viwango vya riba kutoka taasisi tofauti, hivyo kuchagua chaguo bora zaidi kulingana na mahitaji yao. Kwa mfano, benki yenye riba ya 13% kwa mkopo wa miaka 10 inaweza kuwa chaguo la kuvutia kwa mtumishi anayelenga kulipa deni lake kwa muda mrefu.
Hata hivyo, bado kuna maswali kuhusu viwango vya riba, bima za mikopo, na jinsi taasisi fulani zinavyojipambanua sokoni. Kwa mfano, taasisi yenye riba ya 36% bila bima ya mkopo inawavutiaje wateja, na je, wateja wanapata thamani inayolingana na gharama hizi kubwa?
Ni wazi kuwa ushindani kati ya benki na taasisi za fedha unatoa fursa kwa wateja kuchagua huduma bora zaidi. Kama una maoni au uzoefu wa moja kwa moja na mikopo kupitia mfumo wa ESS, usisite kushiriki mawazo yako.
Leave a Comment