Mbosso – Penzi Limevuja tena Lyrics
Oooh, oooh maya aah
(Nusder)
Si umesema mi baniani mbaya
Na uwepo wangu kwako sio dawa, haya aah
Penzi nikashona tenzi na riwaya
Kwenye moyo wako livae liwe sawa, limepwaya
Napuliza majivu maana moto siuoni
Kooni maumivu vumbi larudi machoni
Ahadi za mbivu zimebaki ndotoni
Lile penzi tulivu leo lipo kikaangoni
Imeniponza huruma kirungi
Kujitisha kumsaidia
Kumbe katoboa mtungi
Maji yananimwagikia
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena aah
RELATED: Mbosso – Limevuja
Ulisema sikiwambaza
Penzi letu ukuta wa chuma
Nikitoka kiwalaza
Utanistiri nywele za nyuma
Mara kwa mara ulilia
Kifuani umenilalia
Ukijuta unayachukia
Yale ulopitia
Eti kama mimi hujaona
Wa kufanana naye
Asa mbona hukusema
Kama ushakutana naye
Napuliza majivu maana moto siuoni
Kooni maumivu vumbi larudi machoni
Ahadi za mbivu zimebaki ndotoni
Lile penzi tulivu leo lipo kikaangoni
Imeniponza huruma kirungi
Kujitisha kumsaidia
Kumbe katoboa mtungi
Maji yananimwagikia
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena
Penzi limevuja tena aah
Leave a Comment