Entertainment

Marco wa Zabron Singers afariki dunia

Marco wa Zabron Singers afariki dunia

Mwimbaji wa kundi la Zabron Singers, Marco Joseph amefariki dunia kwa ugonjwa wa Moyo jana usiku akiwa anapatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Shemeji wa marehemu, Tecla Lucas ameiambia Mwananchi leo Agosti 22, 2024 kuwa mwili wa marehemu bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti kwenye hospitali hiyo, wakisubiri ratiba za mazishi kupangwa.

“Amefariki kwa ugonjwa wa moyo akiwa Hospitali ya Muhimbili jana usiku msiba utakuwa Mikocheni kwa mama yake mdogo, mwili kwa sasa bado upo kwenye chumba cha kuhifadhia maiti,”amesema Tecla

Leave a Comment