Bushoke ft Juliana Usiende Mbali Lyrics
Bushoke ft Juliana Usiende Mbali Lyrics -“Wimbo Usiende Mbali” ni wimbo unaoimbwa na Juliana Kanyomozi kwa kushirikiana na Bushoke. Huu ni wimbo unaohusu mapenzi na kumhimiza mpenzi wake asiondoke mbali, akionyesha umuhimu wa kuwa pamoja katika mahusiano.
Bushoke ft Juliana Usiende Mbali Lyrics
Verse 1
Deka unavyo Deka kama mtoto
Natakubembeleza mimi wako
Nita zidi kukupa vitu moto moto
Mapenzi kupendana sii mchezo
Nakusihi usije niacha mimi solemba
Najisihi na mimi nisije kukuacha wewe solemba
Na Tunavyo ishi wanadhani tunadanganyana
Sii rahisi amini mimi na wewe tukatengana
Chorus 2x
Usiende mbali nami
Mimi bado nakupenda
Usiende mbali nami
Mimi bado nakupenda
Verse 2
Tangu niko na wewe ni furaha
Kukosa hata saa ni karaha
Bila wewe siwezi ishi
Kwako mi sio mbishi
Wanapiga misele kila mara
Wanatimua mavumbi sisi twala
Wanataka mapinduzi na mapinduzi hawayawezi ooh ooh
Maumivu ya mapenzi naogopa sana
Hata wivu ninao kwani sina roho ya chuma
Nakusihi usiniacha mimi solemba
Najisihi na mimi nisije kukuacha wewe solemba
Chorus 2x
Usiende mbali nami
Mimi bado nakupenda
Usiende mbali nami
Mimi bado nakupenda
Usiendeeee……mimi bado nakupenda (2x)
Usiondoke…..mimi bado nakupenda (2x)
Nakupenda wanipenda usije kwenda mbali nami
Usiende……mimi bado nakupenda
Usiondoke….mimi bado nakupenda (3x)
Nakupenda wanipenda usije kwenda mbali nami
Leave a Comment