Lyrics

Barakah The Prince – Siachani nawe Lyrics

Barakah The Prince – Siachani nawe Lyrics

Barakah The Prince – Siachani nawe Lyrics “Wimbo “Siachani Nawe” wa Barakah The Prince ni mojawapo ya nyimbo maarufu kutoka kwa msanii huyu wa Tanzania. Barakah The Prince, ambaye jina lake halisi ni Barakah Andrew, amejulikana kwa sauti yake ya kipekee na uandishi wake wa mashairi yenye hisia.

Katika wimbo huu, “Siachani Nawe,” Barakah anaimba kuhusu mapenzi yake ya dhati na ahadi ya kutokuachana na mpenzi wake, hata wakipitia changamoto. Wimbo huu umevutia watu wengi kutokana na ujumbe wake wa upendo wa kweli na wa kudumu. Melodia ya wimbo ni ya kuvutia, na video ya muziki pia imefanywa vizuri, ikionyesha hisia za upendo na uaminifu kati ya wapenzi.

RELATED: Barakah The Prince – Siachani Nawe

Barakah The Prince alitoa wimbo huu ili kuendeleza safari yake ya muziki, akionyesha uwezo wake mkubwa katika kuandika na kuimba nyimbo za mapenzi. Wimbo huu umepokelewa vizuri na mashabiki, na umekuwa na mchango mkubwa katika kuimarisha nafasi yake katika tasnia ya muziki wa Bongo Flava.

Barakah The Prince – Siachani nawe Lyrics

[Intro]
Ohoo weo, ohoo weo
Ouhoo!
Ohoo weo, ohoo weo
Mmhh! mnhh!
Ohoo weo, ohoo weo

[Verse 1]
Wakati nalazimisha moyo kupenda sio kama ninakosea
Ipo sababu ya mi kurejesha namba ambayo ilipotea
Hali ya mtoto kumsusa mama akishachapwa
ni sawa na mapenzi
Ukishapenda unasahau hata kama ulishafanyiwaga ushenzi
Nakumbuka nilijuta sana kupenda penda kusikokua na thamani
Ila hitaji la moyo lalazimisha kurudia zamani

[Chorus]
Ohoo weo, ohoo weo
Mimi bado nina imani
Ohoo weo, ohoo weo
Ipo siku utanipa thamani
Ohoo weo, ohoo weo
Mimi bado nina imani
Ohoo weo, ohoo weo
Jua mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Acha nisote mie
Ila mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Wacha nisote mie

[Verse 2]
Labda juu ya kaburi utanipenda mimi nikiwa sina uhai
Hisia zangu haziheshimiwi najidharau sifai
Heri ya upofu wa macho kwa yale nayoyaona
Umeruhusu mboni zangu mi kumwaga machozi
Yaani ungejua hisia za mapenzi
Kutesa moyo ila bado hazichoshi
Kupendwa sipendwi najua wazi ila bado silithii
Maana kesho nitaurubuni moyo
Unapendwa ila unapimwa
Mi na meno ila najiona kibogoyo
Kweli penzi donda moyo

[Chorus]
Ohoo weo, ohoo weo
Mimi bado nina imani
Ohoo weo, ohoo weo
Ipo siku utanipa thamani
Ohoo weo, ohoo weo
Mimi bado nina imani
Ohoo weo, ohoo weo
Jua mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Acha nisote mie
Ila mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Wacha nisote mie

[Outro]
Jua mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Acha nisote mie
Ila mi siachani nawe
Na sishindani nawe
Maana upo moyoni (ndani eeh)
Wacha nisote mie

Acha nisote mie ehee
Mi sishindani nawe wewe
Mi sibishani na wewe

Leave a Comment