Ally Kamwe amlipua vibaya Mzee Magoma
Ally Kamwe amlipua vibaya Mzee Magoma -Baada ya sakata linaloendelea kwenye Klabu ya Young Africans SC likihusisha baadhi ya wazee wa klabu hiyo na uongozi uliopo madarakani juu ya kesi iliyofunguliwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wazee wa klabu hiyo wamekana kuhuhusika na hilo wengine wakisema hawamtabui Juma Magoma.
Kupitia afisa habari wa klabu hiyo Ally Kamwe amesema; “Nimeona mijadala ya wazee hivi wazee vile, naomba niwaeleze kuwa wazee wa Yanga msimamo wao ni kuunga mkono viongozi wao waliopo madarakani.
“Wazee wa Young Africans SC wanasema hawahusiki na kesi inayoendelea na mjadala uliosambaa mitandaoni wala huyo magoma.
“Hoja zote ambazo nimezisikia leo kwenye Vyombo vya Habari ambazo Wachambuzi na Waandishi wa Habari mmekuwa mkifanya mahojiano na hao wanaojiita Wanachama wa Yanga, ni hoja zisizokuwa na mashiko hata kwa asilimia 0, ni hoja za hovyo
“Katiba ya Yanga imeanzia kwenye hatua ya matawi, wewe kama ni Mwanachama wa Yanga una haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa tawi, Yanga ina Wachama elfu 80 haya tuamue wote twende Mkutano Mkuu, tunachukua eneo gani?, tunawaweka wapi Watu elfu 80?
“Mabadiliko haya lazima tuyakubali, na mabadiliko haya yamekuja na neema, anaibuka tu Mtu wa hovyo kwasababu tu mirija imekata kidogo, riziki hazipatikani, basi eeh aah aah,, Yanga hiyo haipo, na hauna hiyo nafasi.
“Kama kuna mahala Katiba ya Yanga imebagua ni kutenganisha Watu wa maana na Watu wa hovyo, hatuwezi kuwa na Watu wa hovyo tukawaza mambo makubwa, haiwezekani Watu watatu au wanne wakaumiza Watu milioni 45,” amesema Kamwe.
Juma Magoma ambaye aliwahi kuwa mwanachama wa klabu hiyo kupitia tawi la Magomeni Makuti miaka minne iliyopita huku akisifika kuingia kwenye migogoro mara kadhaa na viongozi wa klabu hiyo.
Leave a Comment