Audio

Nyimbo Za Injili: Mdundo Yamshirikisha Christopher Mwahangila Kwenye Mix Maalum Jumapili Hii

Nyimbo Za Injili: Mdundo Yamshirikisha Christopher Mwahangila Kwenye Mix Maalum Jumapili Hii

Christopher Mwahangila ni mwimbaji wa nyimbo za injili maarufu kutoka nchini Tanzania. Amekuwa akihudumu kwa muda mrefu katika tasnia ya muziki wa injili na amepata umaarufu mkubwa kwa ujumbe wa kiroho na sauti yake ya kuvutia. Mwimbaji huyu amerekodi nyimbo nyingi za injili zinazotambulika na kupendwa na wapenzi wa muziki wa injili katika eneo la Afrika Mashariki.

Jumapili hii kupitia kampeni ya Nyimbo za Injili Sundays ndani Ya Mdundo.com, tunamshirikisha mwimbaji Christpher Mwahangili kwa Mix kali kwa jina “Best of Christopher Mwahangila.”-https://mdundo.com/song/1621301

Kampeni hii inalenga kuleta baraka na kueneza ujumbe wa muziki wa nyimbo za injili. Kila Jumapili, tunakuletea orodha ya nyimbo za injili zilizo na ujumbe wa upendo, imani, na matumaini. Tunatumaini kwamba kupitia muziki huu, watu watajikumbusha na kuimarisha imani yao na kupata faraja katika nyimbo hizi za kiroho. Jisikie huru kujiunga nasi kila Jumapili na kufurahia nyimbo hizi za kiroho zinazotuletea pamoja katika imani na matumaini.

Christopher Mwahangila amekuwa akishiriki katika huduma ya injili na amefanya maonyesho mengi ya muziki wa injili, pamoja na kuimba katika ibada na mikutano mbalimbali ya kidini. Ujumbe wa nyimbo zake mara nyingi unahusu imani, matumaini, na maisha ya kiroho, na amekuwa akihamasisha watu kuendelea kumwamini Mungu.


Subscribe ili kupata DJ mixes zaidi hapa: https://mdundo.ws/BekaBlog

Mwimbaji huyu ameendelea kutoa mchango mkubwa katika kueneza injili kupitia muziki wake, na amekuwa chombo cha kiroho kwa wengi wanaomsikiliza.Hivi karibuni aliichai kazi yake mpya kwa jina “Litapita” ambapo aalimshirikisha Paul Siria.