Audio

Mdundo yazindua “Nyimbo Za Injili Sunday Mixes” Afrika Mashariki

Mdundo yazindua “Nyimbo Za Injili Sunday Mixes” Afrika Mashariki

Tunayo furaha kubwa kutangaza kampeni mpya na ya kusisimua kabisa, ‘Nyimbo za Injili Sundays’ mixes, inayoletwa kwako na Mdundo.com.

Kampeni hii inakusudia kuinua na kueneza baraka za muziki wa nyimbo za injili. Kila Jumapili, tunakuletea mchanganyiko wa nyimbo za injili zenye ujumbe wa upendo, imani, na matumaini.

Kwa kushiriki kampeni hii, tunalenga kuwezesha wapenzi wa muziki wa injili kupata upatikanaji rahisi kwa nyimbo za injili za hali ya juu na kuvutiwa na ujumbe wa kiroho uliomo katika nyimbo hizi. Vile vile itawahusisha wasaniii mbalimbali tajika walio kwenye mtandao huu ili kuwezesha kampeni hii kuwafikia mashabiki wote.

Kampeni hii itajumuisha wasanii wako wa injili wanaopatikana kwenye Mdundo. Hii itasaidia kuwafikia wafuasi wengi zaidi wa wasanii ambao tunakusudia kuwaonyesha, ambao ni pamoja na Christina Shusho wa Tanzania,Goodluck Gozbert. Kutoka Kenya, tunao Moji Short Babaa, Janet Otieno, Mercy Masika, na wengine kutoka Uganda.

Mdundo.com inajivunia kuchangia katika kueneza injili kupitia sanaa na muziki wa injili ni mojawapo ya njia muhimu zaidi za kufanya hivyo.

Subscribe ili kupata DJ mixes zaidi hapa: https://mdundo.ws/BekaBlog

Tunawaalika nyote kujiunga nasi kila Jumapili kwa burudani ya kiroho na muziki mzuri wa nyimbo za injili. Pamoja, tunaweza kueneza ujumbe wa upendo na tumaini katika ulimwengu wetu.

Karibu kwenye ‘Nyimbo za Injili Sundays’ mixes, na tujenge pamoja jamii ya muziki wa injili iliyo imara na inayokua. Asante kwa kuendelea kutuunga mkono!”

Kwa maelezo zaidi kuhusu kampeni hii, tafadhali tembelea Mdundo.com.