News

WAKILI JOYCE MWAIKOFU AFUNGUKA UMUHIMU WA MALEZI BORA KWA MTOTO NA KUMLINDA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Dodoma.Watoto ni kundi ambalo haliwezi kujitetea pale linapokutana na Ukatili wa aina yoyote, mara nyingi hadi Watu wazima wagundue unakuta Mtoto ameshaathirika Kimwili au Kisaikolojia

Athari za Mtoto kuathirika Kisaikolojia ni kubwa na zinaweza kumuathiri hata akiwa Mtu mzima, hivyo ni vyema kusaidiwa mapema ili kumuepusha na athari za mbeleni

Kwa upande wake Wakili Joyce Mwaikofu alisema Ni vema Kama wazazi/walezi kukaa karibu na watoto wao ili kujua changamoto mbalimbali wanazo kabiliana nazo na kupata ufumbuzi wa kuwasaidia kisaikolojia

Mimi maranyingi sipo nyumbani kutokana na majukumu ya kikazi niliyonayo kwasasa lakini ninapopata nafasi ya kukaa na familia yangu lazima niwahoji watoto wangu wamekutana na Nini wakati Mimi mama yao sipo

Matukio mengi Kama ya ulawiti,ushoga na usagaji yanawapata watoto Ni kwasababu wazazi wengi tuko busy na Mambo yetu niwakumbushe wamama wenzangu tuwafundishe watoto maadili mema na kuwalea katika misingi ya Neno la Mungu ndipo tutakisaidia kizazi hiki Alisema Joyce Mwaikofu

Hivyo Kama jamii Ina wajibu mkubwa wa kukemea mmomonyoko wa maadili unaoendelea kukitafuna kizazi hiki .

Ni vema kutoa taarifa mapema pindi tu inapoonekana mtoto amefanyiwa ukatili Kama vile kubakwa ,kurawitiwa na taarifa kufikisha katika kituo Cha polisi na ustawi wa jamii