Lyrics

Moyo Wangu by Patrick Kubuya Lyrics

Moyo Wangu by Patrick Kubuya Lyrics

Moyo wangu, usilie tena
Moyo wangu, usibabaike
Unaye Mungu, mkuu sana
Unaye Mungu, muweza wa yote

Refrain:
Aliingia moyoni mwangu
Kanipa kutulia
Kaniambia “ewe mwanangu
Usilie lie tena
Ninajua shida zako
Mimi nitazitatua”
Bila Yesu, mimi ni mtu bure
Bila Yesu, mimi ni mtu bure

Kati giza, Yesu ni mwanga
Kati huzuni, Yesu ni mfariji
Kati vita, Yesu mwamba
Katika njaa, Yesu ndiye mkate
Yesu kimbilio, hajawahi kuniacha
Yesu mwamba wangu, mahali pa kujificha
Yesu kimbilio, hajawahi kuniacha
Yesu mwamba wangu, mahali pa kujificha
Anajua shida zangu, Yeye atazitatua
Bila Yesu, mimi ni mtu bure
Bila Yesu, mimi ni mtu bure

Refrain
Ndani ya Kristo ninaweka tumaini langu
Sijui bila wewe Bwana wangu
Ningekuwa wapi
Eh Yahweh, we ni yote kwangu?

Eh Yahweh, we ni yote kwangu
Eh Yahweh, ningekuwa wapi?
Eh Yahweh, we ni yote kwangu
Eh Yahweh, ningekuwa wapi? (Repeat)