Audio

Mixes 3 Kali Za Mapenzi Kipindi Hiki Cha Valentines

Siku ya Valentine al maarufu kama Valentines day ni siku ya kipekee ambayo utapata nafasi ya kuonesha upendo kwa yule umpendaye.

Kuna njia ipi nyingine bora ya kuonesha upendo wako kwa umpendaye zaidi ya kumtumia ngoma ambazo zitaonesha hisia zako? Kuanzia ngoma za mapenzi kutokea Bongo kwenda kwenye ngoma za Afrobeats, tumekukusanyia mixes 3 kali kwa ajili yako katika kipindi hiki cha Valentines.

  1. African Love Mix

Mix hii itakupeleka kwenye safari ya kimuziki kutokea Mashariki, kwenda Magharibi mpaka Afrika Kusini ikiwa na wasanii kama Diamond Platnumz, Nasty C, Black Coffee na Tiwa Savage.

  1. Afrobeat Love Mix

Mix hii ya Afrobeat itajenga hali yako ya hisia kuwa bora sana katika usiku wa wapendanao ukiwa na mpenzi wako huku ikiwa imeshirikisha wasanii kama Guchi, Rema, Omah Lay, Ckay na Nandy.

  1. Bongo Valentines Love Mix

Wanasema Kiswahili ni lugha ya mapenzi na mix hii itakusaidia kueleza hisia na upendo wako kwa mpenzi wako katika siku ya Valentine ukiwa na rafiki yako. Mix hii imeshirikisha wasanii kama Nadia Mukami na Otile Brown, Billnass, Barnaba Classic na Ali Kiba.

Bonyeza hapa kupata DJ mix nyingine zaidi: https://mdundo.ws/edu_tz