Jinsi ya kupika Maandazi
Jinsi ya kupika Maandazi – Nimekuwea Mapishi murua ya Maandazi, fuatisha hatua kwa hatua ili uweze kutengeneza Maandazi laini kabisa.
MAHITAJI YA MAANDAZI
1. Unga – 5 Vikombe.
2. Tui la Nazi zito vugu vugu – 1 ¼ kikombe.
3. Sukari – 3/4 kikombe cha chai.
4. Samli iliyoyayushwa au mafuta – 3 vijiko vya Supu.
5.Hamirah – 2 Vijiko vya Supu.
6. Hiliki – 1/2 Kijiko cha chai.
7. Mafuta ya kukaangia.
RELATED: Jinsi Ya Kupika Ugali | How to Cook Ugali
Jinsi ya kupika Maandazi
NAMNA YA KUTAYARISHA NA KUPIKA.
1. Ndani ya kibakuli kidogo, mimina hamira na na vijiko viwili vya kulia vya tui. Weka kando mpaka hamira ianze kufura, kama dakika 5-10.
2. Pasha samli moto:
3. Ndani ya bakuli kubwa au sinia, changanya unga, sukari, iliki na samli ikiwa bado moto moto.
4. Mimina hamira ndani ya mchanganyiko wa unga.
5. Changanya na ukande huku ukitumia lile tui la nazi. Tui likipungua unaweza ukaongeza maziwa.
6. Kanda unga mpaka uwe laini.
7. Kata madonge *12 au 15 uyaweke kwenye baraza iliyonyunyiziwa unga na uyafunike ili yapate kufura na yasikauke.
*Ukipenda maandazi manene fanya madonge 12. Ukipenda mepesi fanya madonge 15.
8. Madonge yakifura, sukuma kama chapati kisha ukate mara nne kama kwenye picha. Endelea kufanya hivyo na madonge yote. Yawache maandazi yafure tena baada ya kukata kama dakika 15 hivi.
9. Pasha mafuta moto kwenye karai. Maandazi yako tayari kukaangwa sasa.
10. Kaanga maandazi kwenye mafuta ya moto. Upande mmoja ukifura na kuwa rangi nzuri geuza upande wa pili. Endelea nama hii mpaka maandazi yote yawe tayari.
Jinsi ya kupika Maandazi
Vidokezo: Kuhifadhi Maandazi:
Unaweza kuweka unga wa maandazi uliyokwisha kuyakata ndani ya freezer yakisha umukua ikiwa unataka kutumia siku nyengine.
Tumia waxed paper na unga wa kutosha kuweka katikati ya maandazi ili yasishikane unapoya freeze kwanza katika freezer.
Yakishika barafu, toa na yafunike kwa wax paper kiasi kama matano pamoja na uyatie katika freezer bags. Ukitaka kukaanga maandazi siku nyengine, toa maandazi mapema kidogo yatoke barafu kidogo tu.
Pasha mafuta moto kwenye karai na kanga maandazi.
Vile vile unaweza kuyapika kabisa na kuweka katika freezer bags, ukitaka kutumia ni kuyatoa tu na kupasha moto katika Microwave.