Wasifu wa DJ Massu, Kazi na Show Zake Kubwa
DJ Massu ni nani na ana miaka mingapi?
Jina la usani: DJ Massu
Jina halisi: Athuman Kassim Swahib
Mix tapes zake ni za muziki gani: Bongo, Hiphop, RnB
DJ Massu alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?
Athuman Kassim Swahib almaarufu DJ Massu alianza kazi ya kuwa DJ rasmi mwaka 2007 huko Tanga,Tanzania. DJ Massu kwa sasa ana ujuzi wa zaidi ya miaka kumi na mitatu kwenye fani yake ya kucheza mziki. Katika kazi yake ya usanii wa kuwa DJ, amecheza katika klabu tofauti nchini Tanzania.
Massu amefanya Kazi na Radio gani?
Kandona kucheza muziki kwenye vilabu, DJ Massu amepata fursa ya kufanya kazi na vituo mbali mbali vya radio kama vile, Nyemo FM (Tanga ) na kwa sasa anafanya kazi na kituo cha A-FM iliyoko Dodoma tangia mwaka 2015.
Radio Shows zake ni kama zipi?
- Kipindi cha Kazi na dawa Fast
- Kipindi cha The Finest
- Kipindi Sport na Music
Mbali na kufanya kazi kwenye radio, DJ Massu anafanya kazi kama mkuu wa idara ya burudani na usimamizi wa maDJ katika hoteli ya Royal Village iliyoko Dodoma.