LEARNING

Jinsi ya kutengeneza Batiki

Jinsi ya kutengeneza Batiki

Jinsi ya kutengeneza Batiki -Jinsi ya kutengeneza batiki ya kufunga kwa kamba hatua kwa hatua👇👇

Andaa kitambaa cha batiki kisha kitandike juu ya meza au sakafu  kisha kunja kitambaa hicho kulingana na aina ya mauwa unayoyataka kisha kifunge kamba kulingana na jinsi ulivyokunja

Chovya kwenye rangi kitambaa hicho kulingana na mauwa unayoyataka

Kiache kwa dakika 5-10 kisha fungua kamba anika kivulin kwa dakika 5-10

Fua kitambaa hicho anika kivulin had kikauke  kisha piga pas na kitakuwa tayar kwa matumizi

Jinsi ya kutengeneza Batiki

Baadhi ya mauwa yatokanayo na batiki ya kufunga kwa kamba:

Nyota
Kashata
Sambusa
Mji kati
Misalaba
Misalaba ndani ya drafti
Miraba
Mbavu

RELATED: Jinsi ya kutengeneza Uso uwe Soft

   Malighafi zinazotumika kutengeneza batiki

Kitambaa kiwe cha pamba

Sodium hydrosulfet
Caustic soda
Rangi
Mkasi
Kamba
Maski
Gloves

Jinsi ya kuchanganya rangi

Andaa chombo cha plastic kisha tia

Costic soda vijiko vitatu vya chakula

Sodium hydrosulfet vijiko 3 vya chakula

Rangi vijiko 3 vya chakula

Maji ya moto lita 3
Maji ya baridi lita 2 kisha koroga kwa dakika moja na rangi itakuwa tayar kwa matumizi

NB:angalizo unapochanganya dawa na rangi hakikisha umevaa maski na gloves kwasababu hiz ni chemical