Jinsi ya kutengeneza Batiki
Jinsi ya kutengeneza Batiki -Jinsi ya kutengeneza batiki ya kufunga kwa kamba hatua kwa hatua👇👇
Andaa kitambaa cha batiki kisha kitandike juu ya meza au sakafu kisha kunja kitambaa hicho kulingana na aina ya mauwa unayoyataka kisha kifunge kamba kulingana na jinsi ulivyokunja
Chovya kwenye rangi kitambaa hicho kulingana na mauwa unayoyataka
Kiache kwa dakika 5-10 kisha fungua kamba anika kivulin kwa dakika 5-10
Fua kitambaa hicho anika kivulin had kikauke kisha piga pas na kitakuwa tayar kwa matumizi
Baadhi ya mauwa yatokanayo na batiki ya kufunga kwa kamba:
Nyota
Kashata
Sambusa
Mji kati
Misalaba
Misalaba ndani ya drafti
Miraba
Mbavu
RELATED: Jinsi ya kutengeneza Uso uwe Soft
  Malighafi zinazotumika kutengeneza batiki
Kitambaa kiwe cha pamba
Sodium hydrosulfet
Caustic soda
Rangi
Mkasi
Kamba
Maski
Gloves
Jinsi ya kuchanganya rangi
Andaa chombo cha plastic kisha tia
Costic soda vijiko vitatu vya chakula
Sodium hydrosulfet vijiko 3 vya chakula
Rangi vijiko 3 vya chakula
Maji ya moto lita 3
Maji ya baridi lita 2 kisha koroga kwa dakika moja na rangi itakuwa tayar kwa matumizi
NB:angalizo unapochanganya dawa na rangi hakikisha umevaa maski na gloves kwasababu hiz ni chemical