Audio

Wasifu wa DJ YLB, Kazi Yake Kwenye Wasafi Media na Show Zake

Wasifu wa DJ YLB, Kazi Yake Kwenye Wasafi Media na Show Zake

DJ YLB ni nani?

Jina la usani: DJ YLB

Jina halisi: Genes Paul Massawe

Mix tapes zake ni za muziki gani: Gospel

DJ YLB alianzaje kazi yake ya kuwa DJ na lini?

DJ YLB alianza rasmi kazi yake ya  kuDJ mwaka wa 2014 Dar Es Salaam Tanzania. Hivyo, anajivunia kuwa na tajriba ya zaidi ya miaka saba katika kazi hii. DJ YLB anatambulika kwa kucheza kwenye vilabu tofauti tofauti Tanzania. Kwa sasa, ni mmoja wa maDJ tajika nchini Tanzania na eneo la Afrika Mashariki.

Kando na kucheza kwenye vilabu, DJ YLB pia amebarikiwa kufanya kazi na stesheni kadhaa za redio na televisheni kama vile; E FM na E TV. Kuna wakati pia alifanya live mix kwenye televisheni ya KTN Kenya. Kwa sasa, DJ YLB anafanya kazi na kampuni ya Wasafi Media.

Show zake kubwa ni kama gani?

  1. Wasafi Sunday Worship
  2. The switch

Kando na kuchapa shows, DJ YLB ndiye mkubwa wa idara ya muziki kwenye Wasafi media. Yeye pia ndiye anayepanga playlists zote zinazotumika na Wasafi TV.

Pakua Mixes kali ndani ya Mdundo