Kutoa huduma ya muziki kwa wateja.
Dar es Salaam, Mei 21, 2021: Vodacom Tanzania PLC ikishirikiana na Mdundo.com wamezindua kifurushi cha muziki kitakachopatikana kwa wateja wote wa Vodacom, kifurushi hiki cha muziki kitawapa wateja wa Vodacom urahisi wa huduma anuwai za muziki kutoka Mdundo ikiwemo mchanganyiko wa muziki mpya uliopangwa pekee kwa ajili ya watumiaji waliolipia huduma hii.
Kupitia huduma ya DJ Mixes, Vodacom Tanzania PLC itaburudisha wateja wa huduma hii na kuwapa uhuru wa muziki wa chaguo lao, kutoka mirindimo ya salsa, rhumba hadi bolingo. Akizungumza wakati wa uzinduzi, huo, Mkurugenzi Dijitali na Huduma za ziada wa Vodacom Tanzania Nguvu Kamando alielezea umuhimu wa kuwa na jukwaa lililosheheni burudani za kila aina.
“Badala ya kuhangaika na kuhama kutoka jukwaa moja la burudani kwenda jingine, Sisi kama kampuni inayothamini dijitali, tuliona umuhimu wa kutengeneza kifurushi kimoja ambacho kitajumuisha aina zote za mirindimo ya muziki, na ndio sababu pia tuliamua kushirikiana na Mdundo.com,” alisema Kamando
Kwa kushirikiana na Mdundo.com, Vodacom Tanzania sio tu itatoa njia mpya ya upatikanaji wa miziki mipya na ya zamani lakini pia itawaburudisha watumiaji wa huduma hii wanaopatikana maeneo mbalimbali nchini.
Kwa upande wake, Mkuu wa Telco kutoka Mdundo.com, Patrick Sampao alielezea kuwa kampuni hiyo inafanya kazi moja kwa moja na wasanii zaidi ya 100,000 wa Kiafrika na inatoa orodha ya nyimbo takribani milioni 1.7 zenye maudhui ya Kiafrika na zile za kimataifa.
“Mdundo ni chapa yenye nguvu sana nchini Tanzania, tunayo furaha kuzindua kifurushi chetu cha kwanza cha muziki nchini. Vodacom ina timu yenye dhamira ya kutoa bidhaa zinazoleta suluhisho jipya katika soko linalolingana na maono ya Mdundo, “Sampao alisema
Mdundo ni huduma inayoongoza ya muziki nchini Tanzania na ina watumiaji wa huduma hii zaidi ya milioni 7 kila mwezi barani Afrika wakati Vodacom Tanzania ni kampuni ya mawasiliano nchini ikiwa na wateja zaidi ya 15.5m.
Ili Mteja ajisajili katika (vifurushi vya muziki vya MDUNDO) anapaswa kubonyeza (* 149 * 01 #) kisha chagua (3 nunua vifurushi kisha bonyeza 2 ambayo ni Intaneti kisha utachagua nambari 6. (Kifurushi cha muziki (MDUNDO) baada ya hapo utalipia kiasi cha kuanzia tshs (100, 500 au 3000), kisha utatarifiwa kwa ujumbe mfupi ukithibitishwa kununua chako. Kifurushi hiki kitapatikana kwa muda wa (siku, wiki au mwezi ).kutokana na uchaguzi wa mteja.
Katika kufanikisha ajenda ya Dijitali, Vodacom Tanzania PLC kupitia kitengo cha Dijitali na Huduma za Ziada (Digital and VAS) inakuja na huduma za kidijitali za aina nyingi zaidi, zenye lengo la kumrahisishia maisha mteja wake, miongoni mwa huduma hizi ni pamoja na ‘Simulizi za Shigongo’ ambayo baada ya kujisajili, mteja anapata kusikiliza idadi ya simulizi za hadithi za Shigongo.
Mwisho …