ALBUM/EP

EP | Mmzy – Ascent

Nyota anayekuja kwa kasi chini ya Lebo ya Kerae Records Akachukwu Emmanuel Uche maarufu kwa jina la MMZY ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8
Ni msanii ambaye anakuja vizuri kupitia Muziki aina ya Afrobeat akiwakilisha nchini Nigeria. Licha ya msanii huyu kuwa na ubora katika uandishi wake, sauti yake ni moja ya kitu kinachomtofautisha na wasanii wengine ambao wamewahi kutokea katika muziki nchini Nigeria.
MMZY ameachia rasmi EP yake ya kwanza iliyopewa jina la ASCENT EP yenye nyimbo 8 huku ikiwa na kolabo mbili akiwa ameshirikiana na msanii wa muziki Teni pamoja na Terri.
ASCENT EP imetayarishwa na watayarishaji watano ambaye ni Masterkraft,Echo The Guru,Cranker Mallo,Blaise Beats,Ozedikuz na nyimbo zote kukamilishwa na mtayarishaji Mix Monster.
Nyimbo zote zimeandikwa na msanii MMZY isipokuwa aliyoshirikiana na Teni pamoja na Terri na bila kusahau wimbo namba 3,4,5,8.
Dominate ni wimbo wake unaofanya vizuri kwa sasa ukiwa unapatikana pia ndani ya EP yake hiyo iliyopewa jina la ASCENT.
Kuwa wa kwanza kusikiliza kazi zote kutoka kwenye EP kupitia vyanzo mbalimbali ikiwemo,apple music,boomplay,spotify,audiomack na youtube.
Kwa taarifa zaidi kuhusu MMZY unaweza kumfuata kupitia ukurasa wake wa Instagram @therealmmzy

STREAM VIA AUDIOMACK