News Promo

Harmonize na Rayvanny: Pakua Mixtape Zao 5 Bora Kwenye Mdundo

Msanii tajika kutoka lebo ya Wasafi Rayvanny na mkurugenzi mkuu wa lebo ya Konde Music Worldwide ni miongoni mwa wasanii wanaofanya vizuri nchini Tanzania. Wasanii hawa walifanya kazi pamoja Harmonize alipokuwa bado kwenye lebo ya WCB, lakini wakaanza kuwa na utatanishi hapo Harmonize alipojitoa na kuanza lebo yake.

Katika nakala hii, tunaangazia mixtapes bora zenye nyimbo za wasanii hawa wawili na kukuachia wewe kufanya uamuzi wa yupi kati yao ndio msanii matata zaidi:

Harmonize Bongo Hits Vol.5

Mixtape hii ina mchanganyiko wa nyimbo kutoka kwa wasanii tajika barani Afrika. Nyimbo za Harmonize zilizoshirikishwa kwenye mixtape ni kama vile; Fall in Love na Good. Wasanii wengine walio na nyimbo kwenye mixtape hii ni kama vile;  Diamond, Yemi Alade, Tanasha Donna mwiongoni mwa wengine.

Bongo Mix _ #01

Mixtape hii ni yenye maudhui ya mapenzi. Wimbo wake Rayvanny ulio kwenya mix hii ni ‘Number One’ aliyoshirikishwa Zuchu. Wasanii wengine walio kwenye mixtape hii ni kama vile; Kidum, Sanaipei Tande, Lady JayDee, Otile Brown na Nandy.

Mdundo Wa Singeli #03 Mix

Mixtape hii ina nyimbo za Singeli zinazovuma nchini Tanzania. Wimbo wa ‘Miss Buza’ uliofanywa na Rayvanny na Dulla Makabila ni miongoni mwa nyimbo kwenye mix hii. ‘Miss Buza’ ni kati ya ngoma bora za Singeli zilizoachiwa Tanzania mwaka wa 2020. Ngoma zingine kwenye mix hii ni kama vile; Mesen Selekta, Msaga Sumu, Shollo ,wamba, Nagwa OG miongoni mwa wengine.

Harmonize, Meddy, Tekno Mix

Harmonize anatawala kwenye mixtape hii akiwa na nyimbo tatu. Ngoma zake zilizo kwenye hii mix ni kama vile; Jeshi, Wife aliomshirikisha Lady Jaydee na Kwangaru aliofanya na Diamond Platnumz.

Krizzbeatz, Diamond, Rayvanny, Harmonize Mix

DJ Bee amefanya kazi nzuri kwenye kazi hii. Mixtape hii na nyimbo bora kutoka kwa wasanii kama vile Diamond, Rayvanny, Harmonize, Krizzbeatz, Masauti, Khaligraph, Joeboy na wengine wengi.