News

Navy Kenzo kuja na Album Mpya Hivi Karibuni

Navy Kenzo kuja na Album Mpya Hivi Karibuni

Kundi maarufu la muziki kutoka nchiniTanzania; Navy Kenzo wanajiandaa kurudi na ujio wa album wao mpya, ya pili miakamitatu badaae baada ya AIM (Above Inna Minute) iliyotoka mwaka 2017.Hitmakers hao wa nyimbo kama KATIKA, KAMATIA, GAME na FELLA wamekuwakimya kwa muda huku wakiachia kazi moja moja bila mashabiki wao kujua mipangoyao kimuziki imekaaje, lakini hivi karibuni watu waliokaribu na wasanii hao

wamesema kuna mengi mazuri ya kutegemea kutoka kundi hilo kwani wapo njiani

kuachia album yao mpya itakayoonyesha madiliko waliyoyafanya kipindi chote cha

ukimya wao.

“Wamekuwa wakishinda studio sana na muda mwingi wamekuwa

wakiutumia kurekodi kazi zao mpya. Awali ilitakiwa watoe EP

Project lakini kila wakikaa na kupitia stock yao ya nyimbo wakajikuta

inawawia vigumu kufanya maamuzi ya kukamilisha EP hiyo na

kuwapa mashabiki project yenye nyimbo chache kwani wanahitaji

kitu kikubwa sana kutoka kwao kama fidia ya ukimya wao. Hivyo

wazo la kutoa EP kama limewekwa pause kidogo. Sasa hivi nguvu

yao kubwa imewekezwa kwenye kuanda a full-project

itakayowaridhisha mashabiki kuwa ukimya wao haukuwa wa

bure…”

Haijawekwa wazi project hiyo itakuwa na nyimbo ngapi au itaitwaje, ila watu walio

karibu na kundi hilo wanasema ni project ambayo itakidhi kiu ya muziki wa Navy

Kenzo uliokosekana kwa muda kidogo:

“Unajua Navy Kenzo sio watu wa kelele nyingi, mara nyingi wao

huacha muziki wao ufanye hiyo kazi kwa niaba yao. Ila kama ni

kurekodi, wanarekodi sana au niseme wamekuwa wakirekodi sana.

Ukikaa studio pale kwa Nahreel huwezi kukosa ngoma kali. Wana

muziki mwingi sana, kila siku wanajaribu kurekodi vitu vipya na

ideas tofauti tofauti mpya ili kupata kitu kilichobora. Hii project

mpya ni kazi kubwa sana; kuanzia sound ya muziki, production,

vibes, na miondoko yake. Wamejitahidi sana. Navy Kenzo wanajua.

Mwaka 2019 ulikuwa mwaka wa mambo mengi mazuri kwa Navy Kenzo, waliachia

nyimbo kadhaa ikiwemo: FELLA yenye views zaidi ya 1,800,000 kwenye mtandao

wa YouTube, MAGICAL yenye views zaidi ya 350,000 na ROLL IT yenye views zaidi

ya 350,000 pia ambazo kazi zote hizi zilikuwa zina ashiria kuwa kundi hilo

linachukua direction mpya ya muziki wao na pengine kulenga zaidi soko la mbele

kitendo ambacho pia kiliwapa fursa ya kushiriki katika festival kubwa ya muziki wa

Africa; AFRO NATION GHANA ambapo matokeo yake yaliwezesha kundi hilo

kutengeneza uhusiano na wasanii wengine wa Africa amabao baadhi yao tunaweza

kuwategemea kuwaona kwenye project yao mpya:

“Ghana ilikuwa experience kubwa sana kwao, connections

walizotengeneza kati yao na wasanii wengine walioenda kushiriki kwenye

festival hiyo inaonyesha ni jinsi gani walivyo na nafasi ya kufanya vitu

vikubwa sana. AFRO NATION GHANA haikuwa tu wao kwenda kuperform

bali kutengeneza pia opportunity za kushirikiana katika kazi za muziki na

wasanii na maproducer wa kule, na imani wachache wao watakuwepo

kwenye album. Wamefanya kitu kikubwa sana kwenye hii project. Hii sio

tu project ya Navy Kenzo, ni project ya mashabiki, wadau wa muziki na

watu wote barani Africa na duniani wanaopenda muziki mzuri, hasa good

African music. Endelea kuwafuatilia utaona.”

Hivi karibuni pia Navy Kenzo kupitia Instgram LIVE yao walikuwa na Mzazi Willy

Tuva mtangazaji maarufu wa redio kutoka Kenya na katika mazungumzo yao

kuchangia ukarabati wa studio ya muziki “8hoodmusic” inayosaidia kuinua Vipaji vya

wasanii waishio kwenye hali na mazingira duni iliyopo Kibera, Kenya; kundi hilo

liliulizwa juu ya mipango yao kwa huu mwaka na kusema wanajuandaa kutoka

project mpya mwezi Juni; – https://www.instagram.com/navykenzo_pr

Navy Kenzo binafsi bado hawajaweka wazi kuhusiana na hili; ila waliokaribu na

kundi hilo wanasema tukae chonjo na tutegemee project mpya kutoka kundi hilo

pendwa la muziki kutoka Tanzania karibuni.

Leave a Comment