LEARNING

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka -Makala hii ni maalumu kwa ajili ya wanandoa tu na si vinginevyo au kama elimu kwa wanandoa watarajiwa. Muogope Mungu uzinzi ni dhambi kubwa sana.
Katika kilele cha juu kabisa cha furaha katika ndoa, kama inavyojulikana, ni sherehe inayopatikana katika tendo lenyewe la ndoa. Ingawa, ili furaha hiyo ipatikane ni lazima tendo hilo liwe limefanyika katika hali ya afya kwa wanandoa wote wawili.


Nguvu za kiume ni neno linalotumika mara nyingi kumaanisha ‘Uwezo wa mwanaume kufanya tendo la ndoa’. Na inapokuwa tofauti na hivi, tunaita ni ‘kupungua au kukosa nguvu za kiume’.
Kupungukiwa kwa nguvu za kiume hutofautiana toka mtu mmoja hadi mwingine. Inaweza kuwa ni hali ya kutokuwa na uwezo wa kusimamisha uume, au hali ya kutokuwa na uwezo wa kufika kileleni kwa muda mzuri wa kutosha.

RELATED: Jinsi ya kupata mtoto wa jinsia ya kiume, ni rahisi sana.


Pamoja na hayo yote, elimu mhimu ambayo mwanaume anatakiwa kuwa nayo, ni kuwa nguvu za kiume hazipatikani kwa kutumia madawa ya kemikali au mahala pengine; bali zinatokana na vyakula tunavyokula kila siku.
Vyakula vya kuongeza nguvu za kiume haraka

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka
Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


1. Ndizi
Wakati unafikiria uwezo wa kufanya vema tendo la ndoa unatakiwa kuwaza juu ya uimara wa misuli ya mwili ambayo inatajwa kuwa ni sehemu kuu na yenye muhimu katika kujamiiana. Kwa msingi huo ulaji wa ndizi mbivu unatajwa kusaidia kujenga misuli mwilini na kumfanya mtu aweze kuwa hodari katika tendo la ndoa. (Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka)


Kuwa na stamina ni muhimu katika ufanyaji mapenzi. Ndizi ni chanzo kikubwa cha vitamin B ambayo husaidia sana katika kuongeza stamina na nguvu mwilini hasa wakati wa kufanya kazi nzito.
Ndizi ina kimeng’enyo cha Bromelain ambacho huongeza nguvu za kiume, ashki ya mapenzi ( libido).


2. Tikiti maji
Matikiti maji ni tunda muhimu sanna kwa kulinda ndoa inatakiwa walau kwa siku upate vipande viwili au vitatu na sasa yapo kwa wingi ushindwe wewe na ni muhimu ukala na mbegu zake.


Tunda hili lina faida nyingi pamoja na kuwa ni chanzo kikuu cha Protini, Mafuta, Nyuzinyuzi, Wanga,Calcium, Phosphorus, Chuma,Vitamin A,B6,C. Potasium, Magnesium, Carotene, anthocyanins na Virutubisho vingine vingi.
Tunda linasaidia kuwa na uwezo mkubwa wa kuimalika kwa misuli na mfumo wa fahamu kufanya kazi zake vizuri na kuondoa katika hatari ya kupata shinikizo la juu la damu .


Faida nyingine 12 za tikiti maji kiafya ukiacha hii ya nguvu za kiume
• Asilimia 92 yake ni maji
• Vitamini A ndani yake huboresha afya ya macho
• Vitamini C ndani yake huimarisha kinga ya mwili,
• Huponya majeraha,
• Hukinga uharibifu wa seli
• Huboresha afya ya meno na fizi
• Vitamini B6 husaidia ubongo kufanya kazi vema
• Hubadilisha protin kuwa nishati
• Chanzo cha madini ya potasiamu
• Husaidia kushusha na kuponya shinikizo la damu
• Hurahisisha mtiririko wa damu mwilini
• Huondoa sumu mwilini
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya mara hivi mara kwa mara.


3. Unga wa Mbegu za maboga
Maajabu mengine ya mbegu za maboga ambayo ulikuwa huyajuwi bado.
Utaniuliza kivipi zinaondoa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume? Kwanza kabisa zinaondoa msongo wa mawazo kitu ambacho ni namba 1 katika kusababisha upungufu wa nguvu za kiume.


Lakini pia zinashusha lehemu (cholesterol), zinatibu kisukari, zinatibu tezi dume (matatizo kama ya ngiri nk), zinashusha kisukari, zina protini nyingi ya kutosha na yenye ubora na mbaya zaidi ni kuwa zina madini ya ZINKI madini mhimu kuliko kitu kingine chochote kwenye upande wa nguvu za kiume na kinga ya mwili.
Bado huelewi? Zina madini ya chuma pia


Uzuri ni kuwa mbegu hizi hazina uchungu wowote, ni tamu kuzitafuna wakati wowote na mahali popote hata ukiwa ofisini unaweza kuwa nazo pembeni unatafuna huku unaendelea na kazi zako.
Sambamba na hilo kama tulivyoona pale juu kwamba zinaongeza maziwa kwa mama anayenyonyesha kwa upande wa wanaume zinaongeza pia uwingi wa mbegu za kiume (sperm count) ukitafuna mbegu za maboga siku mbili tu utaona ukimwaga bao linatoka la kutosha na zito kweli kweli basi ujuwe ni mbegu za maboga hizo.


4. Kitunguu swaumu
Kitunguu saumu kina allicin, kiambato kinachosaidia mzunguko mzuri wa damu kwenye viungo vya uzazi. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu kwenye uume ni sababu kubwa ya kuongeza stamina ya kufanya mapenzi.
Sifa kuu za kitunguu saumu zinazokifanya kuwa na uwezo na faida nyingi mwilini ni kuwa na viasili kadhaa ambavyo vina uwezo tofauti tofauti.


Baadhi ya viasili hivi husaidia kutanuka kwa mishipa ya damu ( vasodilation kwa lugha ya kiingereza) kwa kubadilisha polysulphides zilizo ndani yake kuwa hydrogen sulphides kwenye seli nyekundu za damu.
Pia, kitunguu saumu husaidia kuthibiti kiwango cha kemikali iitwayo homocystine
mwilini na hivyo kupunguza madhara ya kisukari. Kitunguu saumu kina allicin , kiambato ambacho husaidia mwili kuwa na mzinguko mzuri wa damu hadi kwenye viungo vya uzazi.


Kuwa na damu ya kutosha katika uume husababisha hiki kiungo kusimama na hivyo kustaimili tendo la ndoa kwa muda mrefu.
Namna ya kutumia kitunguu swaumu:
1. Chukuwa kitunguu swaumu kimoja
2. Kigawanyishe katika punje punje
3. Chukua punje 6
4. Menya punje moja baada ya nyingine
5. Kisha vikatekate (chop) vipande vidogo vidogo sana na kisu na uache hivyo katika hewa kwa dakika 10
6. Meza kama unavyomeza dawa na maji nusu lita kila unapoenda kulala. Namna nyingine nzuri zaidi ni kuviweka ndani ya kikombe kimoja (robo lita) cha mtindi freshi koroga vizuri na unywe na hii itakusaidia kupunguza harufu mbaya ya kitunguu swaumu huku ukipata faida nyingine mhimu zilizomo kwenye mtindi.


Fanya hivi kila baada ya siku 1 unapoenda kulala kwa wiki 3 mpaka 4. Unaweza pia kuendelea kukitumia hata kama unmepona tatizo lako. Ukiona kichwa kizito au kinauma pumzika kutumia kitunguu swaumu kwa siku 3 hivi kisha endelea tena, mhimu usitumie kila siku bali ni kila baada ya siku 1.


5. Siagi ya Karanga
Karanga ni chanzo kikubwa cha kujenga protini mwilini. Karanga huwa na kiwango kikubwa cha amino asidi ambayo husaidia kuweka vizuri mfumo wa damu, hivyo kusababisha kuongezeka kwa kiwango cha ufanyaji mapenzi.
Siagi ya karanga ina kiasi kingi cha mafuta masafi yasiyoweza kusababisha kolesto/lehemu mwilini (unsaturated fats) na kiasi kingi cha protini, vitu hivi viwili vinafanya kazi ya kuongeza nguvu mwilini. Siagi ya karanga ina kalori nyingi zitakazokuwezesha ubaki ni mwenye nguvu kutwa nzima.


Kwakuwa ni chanzo kizuri cha madini ya chuma, shaba, magnesium, na potasiamu, siagi ya karanga ni nzuri sana katika kuuweka katika usawa mzuri mzunguko wa damu mwilini.
Kadharika kiasi kingi cha protini kilichomo kwenye siagi ya karanga kinasadikika kuwa na uwezo wa kuongeza nguvu au uwezo wa mwili na kutengeneza mishipa mingi na imara zaidi.


Kaanga kidogo karanga bila kuziunguza na usizitie chumvi, kisha zimenye au ondoa maganda yake. Saga kwenye blenda huku ukiongeza kidogo kidogo mafuta yoyote ya mboga mboga kama ya alizeti au mafuta ya karanga, ongeza sukari au asali kidogo na chumvi kidogo.
Mimi napenda zaidi kuitumia kwenye mkate lakini pia unaweza kuongeza siagi ya karanga kwenye karibu kila mboga ya majani, samaki na kadharika. Ukiacha radha yake nzuri na tamu, siagi ya karanga ni chakula chenye afya na nguvu nyingi na isiyo na takataka zozote zisizohitajika na mwili.


6. Parachichi
Chakula ambacho husaidia kuongeza uwezo wa mtu kufanya tendo la ndoa ni Parachichi.
Tunda hili linauwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E ambayo husaidia katika uzalishaji wa homoni. Inatajwa kuwa watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwana msisimko mkali wa kimapenzi na kwa upande wa wanawake husaidia kuongezamajimaji yenye utelezisehemu za siri na hivyo kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa kujamiiana.


Hili ni tunda ambalo watafiti wamebaini kwamba lina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume. Tunda hili lina uwezo mkubwa wa kuzalisha vitamini E. Vitamini E husaidia katika uzalishaji wa homoni zinazosaidia kuongeza nguvu za  kiume.
Kulingana na watafiti tofauti, watu wanaotumia tunda hili kwa wingi huwa na msisimko mkali haswa wakati wa kufanya mapenzi. Pia, faida za tunda hili haziengemei upande wa wanaume pekee.


Katika upande wa wanawake, tunda hili husaidia kuongeza majimaji yaliyo na utelezi katika sehemu za siri za mwanamke ili kuzuia uwezekano wa kuchubuka wakati wa tendo la ndoa.


7. Pilipili
Pia pilipili unaweza changanya kwenye chakula au ukala hivyo hivyo kwani zinasaidia mzunguko mkubwa wa damu kwa maana hiyo kufanya kuwa na hisia kali za mapenzi kwa hiyo pili pili ni chachu ya kuuamsha hisia


8. Pweza na chaza
Aina hizi za samaki zinazovuliwa baharini huwa na madini ya zink na chumvi ambayo yanatajwa kusaidia uzalisha wa vichocheo vinavyohamasisha msisimko wa mwili wakati wa tendo la ndoa.
Wataalam na wanasayanzi wa ndani kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili na wa Kimataifa wamethibitisha kuwa supu ya pweza ina uwezo wa kuongeza nguvu za kiume.
Wataalam hao wanadai kuwa supu hiyo inafanya kazi hiyo kwa asilimia kubwa tofauti na madawa mengine ya kemikali.


9. Chocolate
Chocolate inasaidia kuongeza stamina kwenye kufanya mapenzi kwasababu ina viambato vya phenylethylamine na alkaloid. Phenylethylamine ni kiambato kinachopelekea kujisikia vizuri, hasa wakati wa kufanya mapenzi na alkaloid huongeza stamina na nguvu wakati wa mapenzi.


10. Maji ya Kunywa
Inapendeza kunywa maji mengi kwa siku na mtu ajitahidi anywe hata zaidi ya lita tanao kama walivyoshauri wataalam wa mambo hayo.
Maji pia usaidia kuondoa ugonjwa mwilini na homa za mara kwa mara.tikiti majihusaidia kuamasha hamasa mwili.
Kitu gani husababisha uume usimame?


Unaweza kujibu ni msisimko. Ni kweli, Jibu lako linaweza kuwa sahihi. Hata hivyo msisimko ni matokeo. Kipo kinachosababisha kutokea huo msisimko. Bila hicho, hakuna msisimko unaoweza kutokea.
Kila mwanaume anatakiwa kujuwa jibu sahihi la swali hili ili atakapopatwa na tatizo atambuwe wapi pa kuanzia na pa kuishia. Siyo lazima uwe daktari, Elimu ya kutambua mfumo wako wa mwili unavyofanya kazi ni mhimu sana kwa kila mtu na si kwa madaktari pekee kama watu wengi mnavyodhani.


Kutokusoma soma lolote kuhusu miili yetu inavyofanya kazi ndiyo sababu kubwa inayotufanya kuparamia dawa kiholela na hivyo kujikuta tunapata madhara zaidi badala ya kujitibu.


Mzunguko wa damu ndicho kitu kinachofanya uume USIMAME. Na kabla hujaendelea kusoma tambua jambo moja mhimu; ‘’Asilimia 94 ya damu ni maji’’. Hii ni kusema katika kila lita 10 za damu, lita 9 kati ya hizo 10 ni maji. Kwa kifupi maji ndiyo kila kitu mwilini, nakushauri upendelee Kunywa maji bila KUSUBIRI KIU.
Mzunguko wa damu unaofanya kazi vizuri kama inavyotakiwa na usio na hitilafu yeyote ni kipengele mhimu sana katika afya ya mwili, mishipa na kusimama kwa uume wako.


11. Pomegranate
Ni aina fulani ya matundamekundu yanayofananana na apple. Haya yatajwa kusaidia kuamsha mishipa ya fahamu na kuweka mawasiliano sahihi ya mwili na hivyo kumuongezea mtu uwezo kwa kufanya tendo la ndoa kwa hamasa kubwa.


12. Mvinyo mwekundu (Red Wine)
Mvivyo mwenyekundu unatajwa kuwa na uwezo wa kuuchangamsha mwili na kuongeza msukumo wa damu, kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya tendo la ndoa, hivyo ni muhimu kunywewa hasa na wale ambao wanasumbuliwa na tatizo la kushindwa kurudia tendo.


Utafiti umedhihirisha kuwa mvinyo mwekundu una wezo wa kuongeza msukumo wa damu. Elewa kwamba kiwango cha msukumo wa damu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa uume umesimama wakwati wa kujamiiana.
Pia, mfinyo mwekundu huuchangamsha mwili kiasi cha kumuondolea mtu uchovu kabla na baada ya kufanya mapenzi.


13. Blueberry
Blueberry ni matunda yanayosaidia sana kuongeza nguvu za kiume, wengi hupendelea kuyaita ‘viagra’ asilia kutokana na kazi inayoifanya mwilini. Blueberries ina virutubishi vinavyoimarisha mishipa ya damu na kusaidia mzunguko mzuri wa damu mwilini.
Damu ndio kila kitu katika nguvu za kiume. Vilevile, blueberries zina nyuzinyuzi ( fiber ) ambazo husaidia kuondoa kolesteroli (Cholestrol) mwilini kabla hazijanganda kwenye mishipa ya damu. Kuwa na mzunguko mzuri wa damu husaidia mwanaume aweze kuhimiri mapenzi wa muda mrefu zaidi.


14. Mtini (Figs)
Mtini (figs) ni matunda yenye kiwango kikubwa cha amino asidi, ambayo ni kiungo kikubwa katika kuzalisha homoni mwilini. Homoni ndio kishawishi cha nguvu za kiume mwilini. Kukosa amino asidi huweza kusababisha kukosa hamu ya mapenzi au kupungukiwa na nguvu za kiume.


15. Chaza/Kombe wabichi (Raw Oysters)
Chaza wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc. Madini za zinc hutumika katika utengenezaji wa homoni ya testosterone, shahawa na mbegu za kiume. Uwingi wa uzalishwaji wa testosterone mwilini huathiri pia hamu ya mapenzi na nguvu za kiume – ikiwa kidogo huondoa hamu, ikiwa nyingi hupelekea hamu na nguvu zaidi.
Kupungukiwa kwa madini ya zinc husababisha kupungua kwa nguvu za kiume, udhaifu (uhanithi), na kushuka kwa kiwango cha uwezo wa kufanya mapenzi.


16. Tangawizi
Tangawizi Ni Moja Ya Chakula Kinachoweza Kurejesha Nguvu Za Kiume, Unaweza Kuichemsha Tangawizi Na Ukatumia Kwa Kuinywa Kama Chai Asubuhi, Mchana Na Jioni Pia Tangawizi Unaweza Ukaitumia Katika Mchanganyiko Wa Kiasili Kwa Kutumia Habat Soda, Asali, Kitunguu Swaumu Na Tangawizi Yenyewe.


Tangawizi husisimua sana mfumo wa mzunguko wa damu mwilini. Kwa hivyo, ni bayana kuwa kiungo cha mwanamume kinachoshiriki tendo la ndoa kitakuwa na damu ya kutosha na pia kusimama kwa muda mrefu. Pia, ulaji wa tangawizi husaidia kuongeza hamu ya tendo la ndoa.
Chukua Tangawizi Na Kitunguu Saumu Vitwange Kisha Vichanganye Na Asali Pamoja Na Unga Wa Habat Soda Na Uwe Unakunywa Mchanganyiko Huu Kwa Kutumia Kijiko Cha Chai Kimoja Kutwa Mara 3 Kwa Muda Wa Wiki Moja Na Utaona Mabadiliko.


17. Asali
Asali ina madini yanayoitwa boron, ambayo husaidia mwili kutumia homoni ya estrogen ambayo ni homoni inayohusika na viungo ya uzazi na mapenzi kwa mwanamke.
Pia kuna utafiti unaoonesha kwamba asali huongeza nguvu, kitendo ambacho kitapelekea mwanamke kuwa uwezo na hamu ya tendo la ndoa au libido.


18. Oysters
Huwa na kiasi kikubwa sana cha madini ya
zinc na haya madini ndiyo huhusika zaidi na uzalishaji wa homoni ya testosterone kwa wanaume.
Pia imethibitika kwamba wanaume wenye ukosefu wa madini ya zinc huwa na matatizo ya nguvu za kiume na wakati huohuo kuwa na madini mengi ya zinc mwilini huongeza kiwango cha shahawa.


19. Ugali wa dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume.
Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake.
Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.


20. Kahawa
Kutumia kahawa kupita kiasi kunaweza kusiwe kuzuri kwa afya yako.Lakini hatukatai kwamba kafeini iliyomo kwenye kahawa inaweza kukupa nguvu nyingi sana za kuweza kuchelewa kufika kileleni mapema.Tumia kinywaki hiki kwa busara kwani kinaweza kikawa kina faida na hasara kwa upande mwingine pia.


21. Zabibu
Kemikali ya anthocyanins iliyomo kwenye zabibu husaidia kwa kiasi kikubwa sana kuisafisha mishipa ya ateli na hivyo kufanya mazunguko wa damu kuwa mzuri hasa katika sehemu za uume wako.Hii ni kwasababu mishipa ya damu inakuwa imefunguka na damu kutiririka vizuri katika maeneo hayo.


22. Mayai
Mayai yanachukuliwa kama mbadala wa uhakika zaidi katika kuongeza uwingi wa mbegu pamoja na kuongeza spidi au kasi yake. Yana vitamini E nyingi na protini ya kutosha vitu viwili mhimu katika kuongeza mbegu.
Mayai yanafanya kazi nyingine mhimu nayo ni kuzilinda seli za mbegu za kiume kutoshambuliwa na vijidudu nyemelezi kirahisi ambavyo vinaweza kuwa sababu ya kupungua kwa mbegu zako.


Viinilishe vilivyomo kwenye mayai vinafanya kazi ya ziada ya kuzifanya mbegu zenye afya zaidi na zenye nguvu zaidi jambo ambalo ni mhimu kwa ajili ya uzazi kwa upande wa mwanaume.
Kumbuka ni mayai ya kuku wa kienyeji tu yanayofaa kwa kazi hii. Kila siku kula mayai mawili mpaka matatu kama una tatizo hili la kuwa na mbegu chache.


23. Spinach
Folic asidi ni kitu mhimu katika kuongezeka kwa mbegu za kiume. Spinachi na mboga nyingine za majani zenye rangi ya kijani ni mhimu kwa ajili hii sababu ya vitamini na kuweka sawa usawa wa ‘folate’ kwenye mfumo wako wa mwili.
Kama folate ipo chini kuna uwezekano ukawa unatengeneza mbegu zisizo na umbile linalotakiwa kwa uzazi na hiyo hupelekea shida na matatizo mengine ya uzazi upande wa mwanamke (birth defects) kama ujauzito kutoka mara tu mimba inapotungwa.


24. Asali yenye mdalasini
Asali ina madini na vitamini nyingi ndani yake, wakati mdalasini wenyewe una kalsiamu, chuma, vitamini C, vitamini K, manganizi na nyuzinyuzi (fiber).
Vinapoungana vitu hivi viwili hufanya dawa moja mhimu sana ya kuongeza kinga ya mwili. Kunywa chai yenye asali na mdalasini mara kwa mara kunaongeza kinga ya mwili, nguvu ya mwili na nguvu ya ubongo kwa pamoja. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 8 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Acha ndani ya bakuli kubwa ili iwe rahisi kuikoroga vizuri kila unapoitumia. Lamba vijiko vikubwa vitatu kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


Hata baada ya mwezi mmoja kuisha bado nakushauri uendelee kuitumia asali hivi maisha yako yote au hakikisha haipiti siku bila kunywa au kula chakula chenye asali yenye mdalasini ndani yake. Unaweza kuitumia kila siku kwenye mkate kama mdabala wa siagi au blueband au ukaitumia kwenye juisi na kwenye chai kama mbadala wa sukari. Au unaweza kuweka vijiko vikubwa vitatu ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote kutwa mara 2 amabapo husaidia pia kutibu uchovu mwilini. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


25. Tumia chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka

Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


NJIA ZINGINE ZA KUONGEZA NGUVU ZA KIUME AMBAZO SIYO CHAKULA


1. Acha mawazo
Msongo wa mawazo
Mawazo na mfadhaiko huondoa mtiririko mzuri wa damu kwenda kwenye uume na kusababisha nguvu kupungua nguvu za kiume na hata uume wenyewe.
Ikiwa unasumbuliwa na mfadhaiko au stress uangalifu mkubwa unahitajika kabla ya kuamua kutumia dawa yoyote. Katika hali ya mfadhaiko wa akili utokanao na hali ya kushuka kwa uchumi kwa mfano, wanandoa wanapaswa kuwa ni wenye umoja na kujaliana zaidi, shida ni pale kama mke akili yake ni ndogo kwani badala ya kufunga na kuomba kwa Mungu huenda akaenda kukutangaza kwa majirani!. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


2. Jitibu magonjwa yafuatayo
Kama tatizo limesababishwa na magonjwa kama kisukari, vidonda vya tumbo, shinikizo la juu la damu au uzito kupita kiasi ni vema ukajitibu kwanza maradhi haya. Tatizo ni kuwa watu wameaminishwa kwamba maradhi haya hayana dawa jambo ambalo si kweli.
Kisukari, shinikizo la juu la damu, vidonda vya tumbo na hata uzito kupita kiasi ni magonjwa yanayotibika kabisa hasa kwa kutumia dawa mbadala na kufuata muongozo sahihi katika kula na kunywa kwa kipindi cha majuma kadhaa.


3. Acha vilevi
Kama tatizo linatokana na matumizi ya vilevi, hatua ya kwanza ni kuviacha kwanza hivyo vilevi. Ndiyo kuviacha kwanza, unatakiwa ujiulize mwenyewe kipi ni mhimu kwako ndoa yako au hivyo vilevi? Mtu anayejali vilevi kuliko hata afya yake hafai.
Kuna watu wanajidanganya kwamba ukitumia sijuwi kilevi fulani nguvu zinaongezeka, ni kweli zitaongezeka hapo mwanzoni mwa matumizi ya hicho kilevi lakini kadri siku zinavyoenda ndivyo utakavyoendelea kuwa mtegemezi wa hicho kilevi na itafika siku hata hicho kilevi hakitasaidia kitu na hapo ndipo hatari zaidi ya kutotibika tatizo lako itakapojitokeza. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


4. Fanya mazoezi ya viungo
Zingatia sana umhimu wa mazoezi ya viungo. Bila kujishughulisha na mazoezi ya viungo kila siku itakuwa ni vigumu sana kwako kupona tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.
Kutengeneza mishipa na kupunguza uzito isiwe ndiyo sababu pekee ya kwenda gym. Kama unahitaji nguvu za kiume na uume wenye afya, unahitaji kujishughulisha na mazoezi ya viungo mara kwa mara ili kusafisha mishipa ya damu na hivyo kuongeza kiasi cha utiririkaji wa damu kwenda kwenye uume.


Kama uzito wako upo juu sana na ni mnene fanya mazoezi ya kukimbia (jogging) kila siku kwa mwezi mmoja mpaka miwili. Kama uzito wako upo sahihi tu kwa mjibu wa urefu wako fanya sana mazoezi ya kuchuchumaa na kusimama. Una chuchumaa na kusimama mara 25 mpaka 30, unaweza kupumzika dakika mbili unaendelea tena kuchuchumaa na kusimama hivyo hivyo unapumzika dakika 2 mpaka mizunguko (rounds) mitano kila siku. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


5. Shiriki tendo la ndoa mara nyingi
Kuna stori zinasema twiga hakuzaliwa na shingo ndefu namna hii kama anavyoonekana akiwa mkubwa, bali wanasema ile tabia yake ya kupenda kula majani ya juu ya miti ndiyo ikapelekea shingo yake ikarefuka!. Inawezekana kuna ukweli kidogo wa stori hizi. Usinielewe vibaya wala usije ukasema huyu jamaa anahamasisha watu kufanya mapenzi! Hapana usiwe na haraka hivyo utanielewa tu ninachotaka kusema


Wanasayansi wa masuala ya mapenzi wanasema ikiwa mtu mzima hana msongo wowote wa mawazo (stress), ana afya nzuri tu ya kutosha na anakula vizuri basi anaweza kushiriki tendo la tendo kila baada ya masaa 24. Angalia na umsome pia mwenza wako pia angalia umri wako, sababu kuna wanawake wengine kwa asili hawapendi kushiriki tendo la ndoa kila mara pia hatuwezi kusema mtu mwenye miaka 50 atakuwa na uwezo wa kushiriki tendo la ndoa kila mara kama mtu wa miaka 18 hadi 40 hivi.


Ni vigumu mtu anakaa mwenzi mzima mwingine miezi miwili mwingine anakaa miezi 6 bila kushiriki tendo la ndoa na utegemee utakuwa na uwezo wa kuchelewa kufika kileleni. Kama hushiriki tendo la ndoa kuna uwezekano mkubwa ukawa unapiga punyeto kitendo ambacho ni kibaya zaidi kwa afya ya uume wako. Kwahiyo unaweza kushiriki mara 2 hadi 3 kwa wiki na unaposhiriki tuliza akili na upate muda wa kutosha wa kuandaana kabla ya tendo na siyo haraka haraka tu (mambo ya short time).


6. Tumia unga wa msamitu
Unga wa msamitu (mtishamba wa porini) ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume hasa lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwa muda mrefu kwani unaimarisha sana mishipa ya uume.


Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari. Msamitu unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama pia.
Msamitu pia unatibu magonjwa yafuatayo bila shida yoyote; pumu, chango la uzazi, kupooza mwili, unaondoa kabisa gesi tumboni na kuongeza nuru ya macho kuona.


Msamitu unao uwezo pia wa kuongeza ukubwa wa uume wako. Labda utauliza kwa namna gani?, kwa sababu moja ya kazi zake mwilini ni kuponya mwili uliokuwa umepooza, mwili unapokuwa umepooza ina maana hata damu yako pia inakuwa haitiririki vizuri kama inavyotakiwa na mzunguko mzuri wa damu una umhimu katika nguzu za kiume.
Kwa kuwa mwili ulikuwa umepooza, Msamitu unapokuja kukutibu unakufanya kuwa mtu uliyechangamka na damu yako itaanza kuwa inatiririka kwa mtiririko mzuri zaidi na kama matokeo yake utaanza kuona hata ukubwa wa mheshimiwa unaanza kuongezeka kidogo kidogo.


Na hii ni hasa kwa wale ambao walizaliwa na uume wa kawaida lakini sababu ya punyeto, lishe duni au stress walijikuta maumbile yao yanaanza kusinyaa au kupungua badala ya kuongezeka. Jinsi ya kuongeza nguvu za kiume kwa haraka


7. Mafuta ya habbat soda
Ukiacha uwezo wake katika kuongeza stamina na nguvu kwa wanaume na kuongeza hamu ya tendo la ndoa kwa wanawake, mafuta haya pia hutumika kutibu tatizo la afya dhaifu la mbegu za kiume na kuongeza wingi wake kwa ujumla (semen count).
Kwa mjibu wa tafiti mbalimbali, mbegu za kiume zinaonekana kuimarika na kuwa nyingi za kutosha baada ya kutumia dawa hii kwa miezi miwili kila siku.
Matumizi : Kunywa kijiko kidogo kimoja cha chai kutwa mara 1 kila siku